October 6, 2024

Mbeki aipa tano Tanzania mapambano dhidi ya utoroshaji fedha

Ni Rais mstaafu wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu lililoundwa na Umoja wa Afrika (AU) kushughulikia tatizo la utoroshaji wa fedha

  • Rais mstaafu wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu lililoundwa na Umoja wa Afrika (AU) kushughulikia tatizo la utoroshaji wa fedha.
  • Tanzania inatajwa kupoteza Dola za Marekani 19 bilioni katika miaka 40 iliyopita katika vitendo vya utoroshaji fedha.

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu lililoundwa na Umoja wa Afrika (AU) kushughulikia tatizo la utoroshaji wa fedha, Thabo Mbeki amesema amepata taarifa na uzoefu kuhusu Tanzania inavyokabiliana na utoroshaji wa fedha katika sekta ya madini, matatizo ambayo yanazikabili nchi zingine Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Mbeki amewaka wazi hisia zake wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli leo 28 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

“Ni wazi kwamba juhudi zinazofanywa na Tanzania zina umuhimu mkubwa kufanywa na nchi zingine za Afrika, kwa pamoja wafrika tunaweza kukabiliana na utoroshaji wa fedha zetu kwenda nje ya nchi zetu,” amesema . Mbeki.

Ripoti ya taasisi ya kimataifa ya Global Financial Intergrity (GFI) ya mwaka 2014 inayohusu tatizo la utoroshaji wa fedha za Afrika inasema Afrika inapoteza Dola za Marekani kati ya 1.4 trilioni na 2.5 trilioni kwa mwaka kutokana na tatizo hilo.

Hiyo ina maana kuwa Afrika imepoteza Dola za Marekani 5 trilioni kwa miaka 50 iliyopita, ikiwemo Tanzania inayotajwa kupoteza Dola za Marekani 19 bilioni katika miaka 40 iliyopita.

Kwa upande wake Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Mbeki kwa kuongoza jopo hilo na kubainisha kuwa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano utakaowezesha kunusuru rasilirnali za Afrika.

Amemshauri kutenga muda ili apate taarifa za uhakika kutoka kwa viongozi na wataalam katika mamlaka zinazodhibiti zinazodhibiti utoroshaji wa fedha hapa nchini.


Zinazohusiana: Wataalam wa benki wapigwa msasa utakatishaji fedha.


Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Nicolai Astrup, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa mchango mkubwa ambao Norway inautoa katika maendeleo ya Tanzania kwenye sekta mbalimbali zikiwemo elimu, kilimo, nishati na gesi.

Rais Magufuli arnemhakikishia Astrup kuwa Serikali  itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Norway ikiwemo kushirikiana na kampuni ya Equinor ya Norway katika uwekezaji wa kiwanda cha kusindika gesi asilia (LNG) kwaa manufaa ya pande zote mbili, na kushirikiana na kampuni ya Yara katika kuwawezesha wakulima kupata mbolea bora na gharama nafuu.

Astrup ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya kupambana na rushwa, kuongezeka kwa ukusanyaji wa kodi na kuimarisha uchumi na kwamba Norway itaendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Amebainisha kuwa pamoja na nchi yake kufadhili  miradi mbalimbali ikiwemo umeme vijijini (REA) na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Norway itatoa Dola za Marekani milioni 56 (sawa Sh127 bilioni) kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mazungumzo kayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba na Balozi wa Norway hapa nchini Elisabeth Jacobsen.