October 6, 2024

Mhadhiri UDSM ateuliwa kuwa mwenyekiti bodi ya NBS

Rais John Magufuli amemteua Dk Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Adrew Masawe aliyemaliza muda wake.

  • Rais John Magufuli amemteua Dk Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Adrew Masawe.
  •  Dk Msengwa alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Dk Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Adrew Masawe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo (Septemba 25, 2019), uteuzi huo umefanyika baada ya Masawe kumaliza muda wake katika kuitumikia bodi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Msengwa alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).