September 29, 2024

Mikopo kwa sekta binafsi yapungua Tanzania

Imepungua hadi wastani wa asilimia 6.2 katika mwaka ulioishia Januari 2021 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

  • Imepungua hadi wastani wa asilimia 6.2 katika mwaka ulioishia Januari 2021 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.
  • BoT katika ripoti hiyo imeeleza kupungua kwa mikopo binafsi kumesababishwa na athari za janga la Corona kwenye shughuli za biashara.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mikopo kwa sekta binafsi imepungua kidogo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, licha ya sehemu kubwa ya mikopo hiyo kuelekezwa katika shughuli za watu binafsi na biashara.

Ripoti ya Tathmini ya Uchumi ya mwezi Februari 2021 (Economic Monthly Review) iliyotolewa na BoT hivi karibuni inaeleza kuwa mikopo kwa sekta binafsi imepungua hadi wastani wa asilimia 6.2 katika mwaka ulioishia Januari 2021 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Uchambuzi zaidi wa takwimu hizo za BoT unaonyesha kuwa mikopo kwa sekta binafsi imeshuka kutoka wastani wa asilimia 10.8 iliyorekodiwa Desemba 2020 hadi asilimia 6.2 ya Januari mwaka huu. 

BoT katika ripoti hiyo imeeleza kuwa kupungua kwa mikopo binafsi kumesababishwa na athari za janga la Corona kwenye shughuli za biashara nchini Tanznaia. 

“Kiwango kidogo cha ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kwa sehemu kinaakisi mgawanyiko katika shughuli za biashara nchini zilizochangiwa na athari za COVID-19,” inaeleza ripoti hiyo. 

Hata hivyo, sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuelekezwa kwa watu binafsi  ambao walipata wastani wa asilimia 34.8 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za biashara zilizokuwa na wastani wa asilimia 15.3. 


Soma zaidi:


Mikopo inayoelekezwa katika shughuli zote kubwa za uchumi imeendelea kuongezeka, isipokuwa kwa shughuli za ujenzi, biashara, kilimo, madini na uzalishaji viwandani. 

Hata wakati mikopo kwa sekta binafsi ikipungua, kiwango vya riba kinachotozwa na benki za biashara nacho kimeshuka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, riba iliyotozwa kwenye mikopo iliyotolewa na benki ilikuwa ni wastani wa asilimia 16.6 mwezi Januari 2021 ikishuka kutoka wastani wa asilimia 16.8 katika kipindi kama hicho 2020. 

Kushuka kwa riba inayotozwa na benki nchi, BoT imeeleza kuwa kumetokana na usimamizi mzuri wa sera za kifedha zinazotekelezwa na Serikali zinazotoa fursa ya kuongeza wigo wa watu kukopa benki ili kuendesha shughuli za kibiashara zinazoweza kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchini.

Mikopo kwa sekta binafsi yapungua Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mikopo kwa sekta binafsi imepungua kidogo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, licha ya sehemu kubwa ya mikopo hiyo kuelekezwa katika shughuli za watu binafsi na biashara.

  • Imepungua hadi wastani wa asilimia 8.6 katika mwaka ulioishia Machi 2020 ikilinganishwa na asilimia 9.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2019.
  • Sehemu kubwa ya mikopo hiyo bado inaelekezwa katika shughuli za watu binafsi na biashara.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mikopo kwa sekta binafsi imepungua kidogo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, licha ya sehemu kubwa ya mikopo hiyo kuelekezwa katika shughuli za watu binafsi na biashara.

Ripoti ya Tathmini ya Uchumi ya mwezi Aprili 2020 (Economic Monthly Review) iliyotolewa na BoT hivi karibuni inaeleza kuwa mikopo kwa sekta binafsi imepungua hadi wastani wa asilimia 8.6 katika mwaka ulioishia Machi 2020 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 9.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2019.

“Hii inaashiria kuwa kwa sehemu kuna pesa za kutosha za kukopesha kutokana na hatua mbalimbali zinachukuliwa na Serikali kuimarisha sera za fedha,” inaeleza ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuelekezwa kwa watu binafsi  ambao walipata wastani wa asilimia 30.2 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za biashara zilizokuwa na wastani wa asilimia 17.7. 


Soma zaidi:


Mikopo inayoelekezwa katika shughuli zote kubwa za uchumi imeendelea kuongezeka, isipokuwa kwa shughuli za hoteli na migahawa, madini na uzalishaji viwandani. 

Hata wakati mikopo kwa sekta binafsi ikipungua, kiwango vya riba kinachotozwa na benki za biashara nacho kimeshuka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, riba iliyotozwa kwenye mikopo iliyotolewa na benki ilikuwa ni wastani wa asilimia 15.83 mwezi Machi 2020 ikishuka kutoka wastani wa asilimia 17.59 katika kipindi kama hicho 2019.

Wiki hii BoT imetangaza  hatua mbalimbali kupunguza makali ikiwemo kuziruhusu benki kujadiliana na wakopaji wao juu ya urejeshaji mikopo ili kupunguza maumivu wakati huu wa mlipuko wa Corona uliosababishwa kuyumba kwa shughuli za uchumi.