July 5, 2024

Mjue askari aliyekataa kubeba silaha vitani na kuokoa watu 75 kwenye pambano kali

Mwanajeshi yoyote  akisikia askari ameenda vitani na amekataa kuua hapana shaka atashangaa sana. Lakini Desmond Thomas  Doss, askari wa jeshi la Marekani aliyekuwa akihudumu kama daktari wakati wa vita ya pili ya dunia (WWII) iliyodumu kuanzia mwaka 1935 mpaka 1945, anajulikana  katika medani za vita kama shujaa wa vita aliyekataa kuua. 

Doss ambaye alikuwa hana silaha hata moja katika uwanja wa  mapambano aliweza kuwaokoa dazani ya askari wenzake katika ya mapambano na hasa pale waliposhambuliwa huko  katika kisiwa cha Okinawa. Matendo yake hayo mema yalimfanya  kuwa askari wa kwanza kupokea medali ya heshimaya  juu katika jeshi la Marekani (Medal of Honor).

Silaha pekee aliyekuwa nayo Doss ilikuwa ni imani yake kwa Mungu na biblia yake ndogo aliyokuwa akiibeba wakati akiwa vitani. Ni imani kubwa ambayo aliyoionesha katika kipindi cha kufa au kupona. 

Mazingira hayo yote yalichochewa na mama yake mzazi ambaye alimlea kuwa Msabato mwaminifu na mtu asiyekula nyama.

Doss  aliyezaliwa Lynchburg jimboni Virginia aliacha shule akiwa mdogo  kwa sababu ya kuwasaidia wazazi wake kipindi cha mwanguko mkubwa wa uchumi ulioanza mwaka 1933.

                                                                                           

Baada ya kutimiza miaka 18 alianza kufanya kazi katika meli ya kivita katika Newport akifanya kazi za ulinzi. Baadaye aliamua kuchukua kozi ndogo ya masuala ya afya lengo lake ikiwa ni kuwasaida watu na wakati wote alikataa kuua adui au kubeba silaha.

Doss alisajiliwa kuwa daktari na kupangiwa katika kikosi namba mbili B ndani ya kikosi cha kwanza cha  miguu namba 307.

Mapambano Okinawa

Wakati wa mapambano huko katika visiwa vya Okinawa juu ya mwamba mwaka 1945, kikosi chao kilikuwa lazima kiupande mwamba maarufu kama Hacksaw Ridge ambapo waliingia katika mtego wa Wajapani.  

Baada ya mapigano makubwa, kikosi chao kiliamariwa kurudi nyuma kwanza wakati huo Doss akiwa ni askari pekee aliyebakia nyuma kwa kuwa hakutaka kuwaacha askari wenzake waliokuwa wamejeruhiwa kwapotee. Alihakikisha anambeba askari mmoja moja aliyeumia mpaka sehemu salama.Aliweza kuokoa askari wenzake wapatao 75 na baadaye aliondolewa Okinawa Mei 21 1945. Mwaka uliofutia kabla ya kuondolewa jeshini aligundulika anaugua ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo alilazwa hospitalini takribani miaka mitano na nusu kabla ya kuruhusiwa mwezi wa nane 1951.

Lakini baadaye ugonjwa uliendelea na kupeleka kupoteza pafu moja na mbavu tano kutokana na kunywa dawa nyingi kupita kiasi na kusababisha awe bubu mwaka 1976.