November 24, 2024

Mshindi wa tuzo Nobel Congo DRC hajajiuzulu kamati ya Corona kulinda jina lake

Hajajiuzulu katika kamati hiyo ili kulinda jina na heshima aliyopewa katika tuzo hiyo, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

  • Ni Dk Denis Mukwege amejiondoa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kupambana na Corona jimbo la Kivu.
  • Hajajiuzulu katika kamati hiyo ili kulinda jina na heshima aliyopewa katika tuzo hiyo, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii. 

Dar es Salaam. Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018 kutoka Congo DRC, Dk Denis Mukwege amejiondoa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kupambana na Corona jimbo la Kivu nchini humo.

Uzushi unaosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kuwa amejiuzulu katika nafasi hiyo kwa sababu kamati hiyo imeshindwa kuwajibika ipasavyo dhidi ya janga hilo na anataka kulinda heshima ya jina lake, siyo kweli.

Habari hiyo imedai kuwa Dk Mukwege hawezi kuchafua sifa aliyoipata kwenye tuzo ya Nobel kwa ajili ya pesa. 

Sehemu ya ujumbe huo ulikuwa katika lugha ya kiingereza ukidai kumnukuu  Dr Mukwege na kueleza  “I cannot in any case dirty my Nobel Peace Prize for money, we had been ordered to declare any illness to be coronavirus and any death.In addition, the thing that displeased me is that, after more than 100 samples none came out positive. I have a career to protect and I am Congolese by blood. Getting rich by lying is a sin before God, I quit.”

Tafsiri isiyo rasmi ni kuwa “Siwezi kuchafua tuzo yangu ya Amani ya Nobel kwa pesa, tuliamriwa kutangaza ugonjwa wowote kuwa ugonjwa wa corona na kifo chochote. Kwa kuongezea, jambo ambalo halikunifurahisha ni kwamba , baada ya sampuli zaidi ya 100 kukutwa na ungonjwa. Nina kazi ya kuilinda na mimi ni Mkongo kwa damu. Kupata utajiri kwa kusema uwongo ni dhambi mbele za Mungu, najiuluzu. ”


Zinazohusiana


Ukweli ni upi

Nukta Fakti imebaini kuwa Dr Mukwege amejiuluzu kweli nafasi yake  katika kamati hiyo lakini kijiuzulu kwake hakuhusiani na sababu zilizotajwa katika habari hiyo. 

Dk Mukwege alitoa taarifa kwa vyombo vya habari Juni 10 akieleza hatua za kujiuluzu kwake kutoka katika nafasi zake za kamati mbili moja ambapo wapo ilikuwa inashughulikia  ugonjwa wa COVID-19 na hakueleza sababu zilizotajwa katika habari ya uzushi iliyoripotiwa.

Sababu kubwa ya kujiuzulu kwa mtaalam huyo wa magonjwa ya binadamu ni kuelekeza nguvu zake katika hospitali ya Panzi iliyopo nchini humo ili kuendelea kutibu wagonjwa wakiwemo wa COVID-19.