Muhogo kinara mazao ya kudumu Tanzania
Ripoti ya Mwaka ya Utafiti wa Sekta ya Kilimo ya mwaka 2016/17 (AAS 2016/2017) iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaonyesha kuwa uzalishaji wa muhogo ulikuwa asilimia 24.2 ya uzalishaji wa mazao yote ya kudumu uliofanyika mwaka 2016/2017.
- Zao la muhogo limetajwa kama zao linaongoza miongoni mwa mazao ya kudumu baada ya takwimu za Wizara ya Kilimo kuonyesha kuwa uzalishaji wa zao hilo ni karibu theluthi moja ya mazao hayo Tanzania bara.
Dar es Salaam. Ripoti ya Mwaka ya Utafiti wa Sekta ya Kilimo ya mwaka 2016/17 (AAS 2016/2017) iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaonyesha kuwa uzalishaji wa muhogo ulikuwa asilimia 24.2 ya uzalishaji wa mazao yote ya kudumu uliofanyika mwaka 2016/2017.
Hiyo ni sawa na kusema karibu theluthi moja ya mazao ya kudumu yaliyozalishwa mwaka huo ulikuwa ni muhogo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa zao hilo la chakula ni Kigoma, Geita na Tanga.