October 7, 2024

Muujiza uliotokea chumba namba saba gerezani

Ni filamu inayomhusu binti mdogo ambaye baba yake ana ulemavu wa akili. Kilele cha filamu hii ni hukumu ya kunyongwa inapotolewa kwa baba huyo kwa kusingiziwa kuua mtoto wa kamanda.
Kilele cha filamu hii ni hukumu ya kunyongwa inapotolewa kwa baba huyo kwa

Filamu ya “Miracle in Cell No.7” itakufunza mambo mengi kuhusu maisha ya familia. Picha|Mtandao.


  • Ni filamu inayomhusu binti mdogo ambaye baba yake ana ulemavu wa akili.
  • Kilele cha filamu hii ni hukumu ya kunyongwa inapotolewa kwa baba huyo kwa kusingiziwa kuua mtoto wa kamanda.
  • Matumaini yanapotoweka, ndipo miujiza inapoanza. Muujiza gani utatokea kwenye chumba namba saba kwenye filamu hii?

Dar es Salaam. “Kichaa, kichaa, kichaa!” ni sauti za watoto wanaomuimbia mwanaume ambaye anacheza nao. 

Kinachoweza kukuvuta zaidi ni kuwa mwanaume huyo ambaye anaimbiwa wimbo huo wa dhihaka na watoto ni baba wa mtoto mmoja wapo. 

“Bibi, baba yangu ni kichaa?” ni swali la mtoto Nisa Aksongur kwa bibi yake Celile Toyon ambaye anamjibu kuwa “Usiseme hivyo binti.” 

“Lakini baba yangu hayupo kama baba wengine,” ni sauti inayomuonyesha mtoto huyo jinsi alivyo kwenye sintofahamu ya uwezo wa kufikiri wa baba yake.

Sintofahamu ya binti huyo inatokana na baba yake Aras Bulut ambaye hayupo vizuri kiakili. Bila shaka watoto wenzie humtania hasa pale baba yao anapokuwa anacheza nao licha ya kumdhihaki kwa nyimbo.


Zinazohusiana


Sintofahamu ya binti huyo na bibi yake inakolea baada ya baba yake kusingiziwa kumzamisha kwenye maji mtoto wa kamanda Mesut Akusta na kuhukumiwa kunyongwa. 

Visa vyote hivyo utavipata kwenye filamu ya “Miracle in Cell No.7”. Una kila sababu ya kuitazama filamu hii yenye kuvuta hisia kama miujiza itamtokea baba huyo aliyeshindwa kujitetea mahakamani kutokana na ulemavu wa akili. Unahitaji kuandaa kitambaa na tishu kwani hakika machozi yanaweza kukutoka kidogo.

“Miracle in Cell No.7” imeongozwa na Mehmet Oztekin utaikuta katika jukwaa la mtandaoni la  Netflix na inashauriwa kutazamwa na watu wenye miaka 13 na kuendelea. 

Ukikamilisha kutazama filamu hiyo, unaweza kugeukia filamu ya “Extraction” ambayo ipo tayari na inangoja utazamaji wako tayari kukutengenezea tabasamu kwenye wikiendi yako.