October 7, 2024

Namna ya kushiriki michezo kwa ufanisi wakati wa janga la Corona

Ni pamoja na kufanya mazoezi binafsi bila haja ya kuambatana na watu wengine.

  • Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, mtu anaweza kuendelea kufanya mazoezi lakini kwa kuchukua thadhari.

Dar es Salaam. Mazoezi ni muhimu kwa kila mtu katika kuijenga afya ya mwili na akili. Hata katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona, bado una uwezo wa kufanya mazoezi ili kubaki fiti na mwenye afya.

Ili kuwa salama, unahitaji kufanya mazoezi na shuguli zako za michezo sehemu ambayo itakuwezesha kujikinga na maambukizi ya COVID-19.  

Unawezaje kubaki na afya yako? Tazama video hii kujifunza.