Ndege ya Air Tanzania kuwarejesha Watanzania waliokwama India
Ndege hiyo inatarajia kutua jijini humo wiki ijayo Mei 11, 2020 na kuanza safari ya kurudi Tanzania siku inayofuata ikiwa na Watanzania hao.
- Ubalozi wa Tanzania nchini India umesema utaomba kibali cha kuiruhusu ndege hiyo kuwasafirisha Watanzania waliokwama nchini humo.
- Ndege itatua katika jiji la Mumbai Mei 11 na kuondoka siku inayofuata.
Dar es Salaam. Ubalozi wa Tanzania nchini India umesema utaomba kibali cha kuiruhusu ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) kutua katika jiji la Mumbai ili kuwarejesha nyumbani Watanzania waliokwama katika nchi hiyo kutokana na kuzuiliwa kwa safari za ndege kulikosababishwa na janga la virusi vya Corona.
Ndege hiyo inatarajia kutua jijini humo wiki ijayo Mei 11, 2020 na kuanza safari ya kurudi Tanzania siku inayofuata ikiwa na Watanzania hao.
Ubalozi huo katika taarifa yake iliyotolewa leo (Mei 7, 2020) umesema hatua hiyo iko katika mpango maalumu unaoratibiwa na Watanzania waishio nchini humo kuwarejesha wenzao nyumbani.
“Ubalozi utahusika katika kuwaombea vibali wale wote watakaokuwa wamelipia tiketi ya ndege hiyo ili waweze kutoka sehemu walipo na kufika Mumbai kwa ajili ya safari hiyo,” imeeleza sehemu taarifa hiyo.
Zinazohusiana
Ubalozi huo umewasisitiza Watanzania wote waliokwama nchini India baada ya kumaliza matibabu na wanafunzi waliopo nchini humo kuchangamkia fursa hiyo.
Ndege itayotumika kwa safari hiyo maalum ni ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania