Ni sahihi kupata chanjo ya Corona ukiwa mjamzito?
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ni sahihi kwa wajawazito kupatiwa chanjo ya Corona kwa maelekezo ya wataalam wa afya.
Dar es Salaam. Kuna maswali mengi kuhusu usahihi wa wajawazito kupata chanjo ya Corona.
Kwa mujibu wa Afisa wa Chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Dk Phionah Atuhebwe, wanawake wajawazito wanaruhusiwa kupata chanjo ya COVID-19 kwa sababu ni salama na inawahakikishia ulinzi dhidi ya ugonjwa huo.
Mazingira gani yanaruhusu wajawazito kupata chanjo?