Kamati yabaini matatizo maabara ya kupima corona Tanzania
Kamati hiyo imebaini kuwa moja ya mashine za kupimia virusi hivyo ilikuwa na hitilafu kwa takriban miezi miwili.
Kamati hiyo imebaini kuwa moja ya mashine za kupimia virusi hivyo ilikuwa na hitilafu kwa takriban miezi miwili.
Kimsingi ujumbe uliowekwa katika picha hiyo hauna uhusiano wowote na watu kuandamana kupinga marufuku ya kutokutoka nje (lockdown) kwa sababu ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona.
Unaweza kuithibitisha habari kwa kutafuta chanzo, kuangalia, lugha iliyotumika na zana za kidijitali ili kujua usahihi wake.
Licha ya kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kushusha gharama za intaneti nje ya bando (vifurushi) bado mtandao huo umeendelea kuwa ghali zaidi ukilinganisha na kampuni nyingine nchini Tanzania.
Bei ya jumla ya mahindi katika Mkoa wa Dodoma imeshuka kwa takriban asilimia 23.7 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linawapa ahueni wanunuzi wa zao hilo katika mkoa huo uliopo katikati mwa Tanzania.
Vicheko vya kuoneana aibu na matembezi ya kudumisha mahusiano vinaendelea kuchagiza penzi la Kumail Nanjiani na binti mwenye ngozi yake, Issa Rae.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema siyo kweli kuoga maji ya moto kunatibu Corona kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amewaambia wanahabari kuwa mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29 Juni 2020 na itafanyika hadi 16 Julai 2020
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania (HESLB) imesema wanafunzi wa vyuo vikuu wataingiziwa mikopo yao ikiwemo fedha za malazi na chakula kabla ya vyuo kufunguliwa tena Juni mosi mwaka huu.
Ni baadaya biashara nyingi za aina hiyo kupumzisha harakati zake ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.
Rais John Magufuli ameagiza vyuo vyote nchini Tanzania kufunguliwa Juni 1, 2020 sambamba na kuruhusu michezo mbalimbali ianze tena siku hiyo.
Wawili hao wataungana na wanamuziki wengine lukuki kutoka bara la Africa kukonga nyoyo za mashabiki wao huku wakionyesha umoja dhidi ya Covid-19.
Kwa sasa watumiaji wa simu za iPhone za toleo la iPgoneX na kuendelea wanapata changamoto ya kufungua simu zao hasa wakiwa wamevaa barakoa.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema ipo tayari kuanza kupokea watalii wakati wowote kuanzia sasa huku ndege ya kwanza ya watalii itawasili mwishoni mwa mwezi Mei.
Rais John Magufuli amesema wamekubaliana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwa mawaziri wa uchukuzi na wakuu wa mikoa wa mipakani wa nchi hizo wakutane ili kumaliza tatizo la kuzuiwa kwa madereva wa malori kupita katika mipaka ya nchi hizo
Thamani ya miamala inayofanywa kupitia huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi imeongezeka kwa Sh711.5 bilioni ndani ya mwezi mmoja licha ya idadi ya watumiaji wa huduma hiyo kupungua.
Baadhi ya wasanii wa Kenya na Tanzania walioshiriki mjadala wa mtandaoni wa kutafuta suluhu dhidi ya athari za COVID-19 katika sanaa hivi karibuni, wameeleza kuwa kwa sasa wasanii wanapaswa kuwa wabunifu zaidi.
WFP imesema watu wasio na uhakika wa chakula katika ukanda huo wataongezeka kati ya milioni 34 na milioni 43 kuanzia mwezi huu wa Mei hadi Julai kutokana na athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19 zimechangia tatizo hilo.
Watumishi waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa Huduma Saidizi, Hans Lyimo, Kaimu Mhasibu Mkuu, Jonas Bakuza na Lecian Mgeta aliyekuwa Mhasibu wa Wakala huo ambaye aliandika barua ya kuacha kazi Aprili 6, 2020.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema thamani ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi katika mwaka ulioishia Machi 2020 imeongezeka kwa asilimia 12.1 yakichagizwa zaidi na bidhaa za mazao ikiwemo korosho na mkonge.