Uber yafyeka wafanyakazi wengine 3,000
Kampuni ya usafiri wa mtandaoni ya Uber imepunguza wafanyakazi wengine 3,000 duniani ikiwa ni hatua iliyochukua kukabiliana na makali ya ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).
Kampuni ya usafiri wa mtandaoni ya Uber imepunguza wafanyakazi wengine 3,000 duniani ikiwa ni hatua iliyochukua kukabiliana na makali ya ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).
Wanahabari wawili kutoka Kenya wanashikiriwa na mamlaka mkoani Arusha wakituhumiwa kuingia nchini na kufanya shughuli za uandishi bila kibali na muda wowote wiki hii watafikishwa mahakamani.
Tanzania imefungua rasmi anga lake ili kuruhusu ndege za kimataifa za watalii na kibiashara kutua nchini baada ya Serikali kusema kuna mwenendo mzuri wa ugonjwa wa virusi vya Corona.
Dk Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema maagizo yaliyotolewa na Rais ni mwongozo utakaofungua fursa kwa Tanzania kuendelea kufaidika na sekta ya utalii.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda nchini Tanzania kuhakikisha wanakata bima ili pale wanapokumbwa na ajali za moto wapate wepesi wa kulipwa fidia za mali zao.
Imeanza kutekeleza agizo lake linalowataka madereva wake kujipiga picha inayoonyesha wamevaa barakoa kabla ya kuwabeba abiria ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona wakati wanatumia usafiri huo.
Amesema amepanga kufungua vyuo iwapo mwenendo wa kushuka wagonjwa wa corona utaendelea wiki inayoanza Mei 18 ikiwa ni miezi miwili tangu vifungwe.
Rasilimali hizo zina mchango mkubwa kwa usalama wa chakula, kuongeza uzalishaji wa mazao na kuhifadhi mazingira.
Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesema hatua hiyo inayoanza kutekelezwa usiku wa Mei 16 itasaidia kudhibiti maambukizi ya COVID-19.
Thamani ya mifugo inayouzwa katika minada mbalimbali nchini Tanzania imeshuka kwa Sh240 bilioni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ikichangiwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Wahudumu hao wa afya wako katika taaluma ambayo inagusa maisha ya watu wengi duniani na hivyo wanahitaji heshima.
Kasi ya ukuaji wa uchumi Tanzania inatarajiwa kukua kwa asilimia nne (4) mwaka 2020 kutokana na athari za ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwenye sekta mbalimbali nchini, ikiwa ni matarajio ya chini ndani ya miaka ya hivi karibuni.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepokea mashine moja ya kupima ugonjwa wa virusi vya Corona kati ya tatu zilizoagizwa nchini Korea Kusini.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 inakadiria kutumia bajeti ya Sh12.39 trilioni huku zaidi ya robo tatu ya fedha hizo zitatumika kulipa deni la Taifa.
Chukua tahadhari ya kuthibitisha habari husika iwapo zimetoka katika tovuti hizo
Sehemu ya ujumbe inasomeka kuwa “Tala imerudi tena kwa mara nyingine baada ya kutotoa huduma kwa muda mrefu” ukiambatana na kiunganishi cha tovuti ambayo mtu akiingia anaweza kupata masharti ya kupata mkopo.
Kuna video zinazosambaa mtandaoni zikionyesha watu wanadondoka na kufariki kwa madai ya kuumwa na wadudu hao.
Serikali ya Tanzania inakusudia kujenga bandari moja ya uvuvi itakayosaidia kuongeza kasi ya uvuvi wa kisasa na biashara ya samaki ili kujipatia mapato na kuboresha maisha ya wananchi wanaotegemea sekta hiyo.
Ni filamu ya “The Wrong Missy” inayosimulia kisa cha mtanashati anayekosea kutuma ujumbe unaomfikia mwanadada ambaye amekuwa akimkwepa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Serikali imekusanya Sh5.5 bilioni hadi kufikia Aprili 30 mwaka huu kupitia operesheni Nzagamba ikiwa ni makusanyo ya tozo za kusafirisha mifugo nje ya nchi.