November 24, 2024

Picha za tetemeko Croatia zilivyotumika kupotosha Corona mtandaoni

Picha hizo zinasambaa kwenye mtandao wa WhatApp zikihushwa na wagonjwa wa corona (covid-19) nchini italia siyo za kweli bali ni za wagonjwa waliokolewa wakati wa tetemeko la ardhi nchini Croatia.

  • Picha hizo zinasambaa kwenye mtandao wa WhatApp zikihushwa na wagonjwa wa corona (covid-19) nchini italia siyo za kweli.
  • Picha za hizo ni za wagonjwa waliokuwa wanahamishwa kwenye hospitali nchini Croatia baada ya kutokea tetemeko la ardhi Machi 22, 2020.

Dar es Salaam.  Ni dhahiri kuwa ugonjwa wa virusi vya Corona unaendelea kuitesa dunia kwa kuharibu uchumi na shughuli za uzalishaji mali. 

Tanzania mpaka jana Machi 31, 2020 imethibitisha kuwa na wagonjwa 19 ambapo mgonjwa mmoja amefariki na mwingine mmoja tayari amepona. 

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za hadi jana Machi 31 zinaeleza kuwa watu 750,890 wameambukizwa ugonjwa huo na kuua watu 36,405 duniani kote.

Licha ya juhudi mbalimbali kutomeza ugonjwa huo, bado baadhi ya watu wanaoutumia ugonjwa huo kutoa habari za uongo kwa nia kuleta taharuki kwa watu, jambo linaloongeza madhara kwa wakazi wa dunia.

Mathalan, March 25, 2020 zilizagaa picha kwenye mtandao wa WhatsApp zinazoonyesha wodi za hospitali nchini Italia zimejaa hivyo baadhi ya wagonjwa  Corona (COVID-19) kutibiwa nje ya hospitali.

 Lakini swali je ni kweli picha hizo ni za wagonjwa wa corona waliopo nchini italia? Hata hivyo, picha hizo  hazitoi habari ya ukweli. Ni uzushi mtupu.

Mfano wa picha iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii hasa WhatsApp ikionyesha hali ilivyo Italia na maneno yanayosema ‘’Hii ni Italia. Hakuna nafasi zaidi katika hospitali. Fikiria mara mbili kabla ya kutoka  nje ya nyumba.’’(This is italy. There is no more space in the hospitals. Think twice before you put your foot outside the house.) lakini kimsingi siyo kweli.

Utafiti wa kihabari uliofanywa na mtandao wa Nukta habari (www.nukta.co.tz) umebaini kuwa picha hizo hazihusiani na wagonjwa wa Corona waliopo nchini Italia bali ni za wagonjwa ambao walitoka nje baada ya kutokea tetemeko la ardhi nchini Croatia.

Nukta imebaini kuwa tetemeko hilo la ardhi lilitokea March 22,2020 katika mji mkuu wa Croatia uitwao Zagred.


Uthibitisho wa mashaka yake

Baaada ya Nukta (www.nukta.co.tz) kufanya tafiti kwa kutumia dhana mbalimbali za kijigitali imebaini kuwa picha zote tano zinatokana na tetemeko la ardhi huko Croatia.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha 5.3 lilisababisha hofu na wagojwa walihamishwa. Wagojwa wanaoonekana wamevaa barakoa ni kwa sababu ya kipindi hiki ambacho mataifa mengi yameathirika na ugonjwa wa COVID-19 ikiwemo Croatia.

Mpaka jana Machi 31, 2020 nchi hiyo ilikuwa na wagonjwa 867 huku sita wakifariki duani na 67 wakipona maradhi hayo.

Ukweli uliopo kwenye picha zote tano 

Picha ya kwanza

 Picha hii ni moja ya picha zinazosamba zikihusisha na wagonjwa wa covid-19 wa nchini Italia lakini Nukta imebaini kuwa picha hii ilitumika kwa mara ya kwanza kwenye tetemeko la ardhi huko Croatia March 22, 2020 kwenye tovuti ya habari ya Total Croatia news unaweza tazama kwa kubonyeza hapa

Picha ya pili

Picha hii inayoonyesha wakina mama wakiwabeba watato wao wachanga mitaani ni ya tetemeko la ardhi katika jiji la Zagreb nchini Croatia na siyo Italia kama inavyosambaa na picha hiyo ilipigwa na Zlatan Jonkovic na kutumiwa katika habari za tovuti ya ABC News March 22, 2020 ikiwa na kichwa cha habari ‘Coronavirus lockdown in Croatia’s capital of Zagreb hampered by magnitude-5.3 earthquake’

Picha ya tatu

Nukta imebaini kuwa picha hii imechukuliwa kutoka kwenye video ya sekunde19 iliyokuchuliwa wakati wa tetemeko la ardhi nchini Croatia ikionyesha watu wakibeba mashine za kuhifadhi watoto wachanga (incubators) ya Adriana Vukovich na unaweza angalia hiyo video hiyo kwa kubonyeza hapa

Picha ya nne

Utafiti uliofanywa kwa kutumia mtandao wa Google unaonyesha kuwa picha hii imetumika na watu mbalimbali  na imetokana na tetemeko la ardhi na iliwekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Angjelina Ahmeti (@angjelinaahmeti).

Picha hiyo ina maelezo kuwa “Uharibifu wa ukubwa wa 5.4 wa tetemeko la ardhi umeipiga Zagreb, Croatia asubuhi hii – ikiwani tetemeko lenye nguvu kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 140! Moyo wangu umeumia kuona wagonjwa na wakina mama wakiwa na watoto walizaliwa kwenye baridi nje wakati huu”

Picha ya tano

Picha hii ilipotafutwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kutumia maneno ya ‘’Hospitali ya Zagreb’ (‘Zagreb Hospital’) ilileta akaunti ya mtandao wa twitter ya mwandishi wa habari Fraser ikiwa na picha hiyo hapo juu na siyo kama invyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni tukio la wagonjwa wa Corona huko nchini Italia.

Picha hizo zote tano hazielezei tukio hata moja la Corona nchini Italia. Kabla ya kusambaza na kutumia picha yoyote kipindi hiki cha mlipuko ni vema ukajilidhisha ili kuepuka upotoshaji.