October 6, 2024

Rais Samia utengua uteuzi wa bosi mpya TPDC

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC), Thobias Richard aliyemteua jana Aprili 4 mwaka huu.

  • Rais  Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Richard aliyemteua jana Aprili 4 mwaka huu.

Dar es Salaam. Rais  Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC), Thobias Richard aliyemteua jana Aprili 4 mwaka huu. 

Rais Samia alifanya uteuzi wa Richard jana na wakuu wa mashirika na taasisi nyingine za Serikali.

Hata hivyo, pasipo kutarajia mapema leo  asubuhi ametengua uteuzi huo na kumrejesha Dk James Mataragio kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo ambaye awali alikuwa anashikilia nafasi hiyo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu Dk Mataragio anaendelea na majukumu yake mara moja.