Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki dunia
amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais mteule Evariste Ndayishimiye.
- Amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais mteule Evariste Ndayishimiye.
Dar es Salaam. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais mteule Evariste Ndayishimiye.
Nkurunziza aliyeiongoza Burundi kwa miaka 15, amefikwa na umauti Jumanne (Juni 9, 2020) katika hospitali ya kumbukumbu ya 50 ya Karusi—Mashariki ya kati ya Burundi–baada ya kulazwa kutokana maradhi ya moyo Juni 8, taarifa ya Serikali iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter imeeleza.
Kiongozi huyo amefariki ikiwa ni takriban wiki tatu tu baada ya nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki kukamilisha uchaguzi mkuu ulioshuhudia jenerali wa zamani wa jeshi Ndeyishimiye akishinda kwa asilimia 68.7 ya kura zote.
Soma zaidi:
- Mengi kuwekeza Sh68 uchimbaji mafuta, gesi Tanzania
- Rais Magufuli, watanzania wamlilia Mengi
- Mengi alivyoacha alama ya uwekezaji katika teknolojia Tanzania
Ndayishimiye aliteuliwa na chama tawala nchini humo cha CNDD-FDD kuwania nafasi hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wagombea wengine saba katika uchaguzi uliofanyika Mei 20.
Nkurunziza (55) alikuwa akitarajiwa kukabidhi madaraka hayo kwa kiongozi huyo mpya mwishoni mwa Agosti 2020 baada ya kukamilisha kipindi chake cha uongozi.
Kipindi cha mwisho cha utawala wa Nkurunziza kilitawaliwa na mivutano ya ndani ikiwa ni tofauti na siku za awali alipotwaa madaraka hayo mwaka 2005.