October 6, 2024

Ripoti ya CAG katika namba

Mambo muhimu yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu matumizi ya fedha za umma katika taasisi za umma katika namba.

  • Mambo muhimu yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu matumizi ya fedha za umma katika taasisi za umma katika namba.

Dar es Salaam. Tangu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/20 itolewe hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali ndani na nje ya mtandao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyoibuliwa katika taasisi mbalimbali za Serikali. 

Nukta Habari (www.nukta.co.tz) tumeisoma na kukuandalia infografia ambazo zimeangazia baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukupa mwanga wa alichozungumzia CAG Charles Kichere katika ripoti hiyo. 

Fahamu kuwa ripoti ya CAG imegawanyika katika maeneo makuu matano: ripoti ya hesabu za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, miradi ya maendeleo, mifumo ya tehama kwenye taasisi za Serikali, mashirika ya umma na ukaguzi wa ufanisi. 

Infografia hizi zitakufungua macho kufahamu kinachoendelea kwenye ripoti hizo kuhusu matumizi ya fedha za umma:

1. Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR nao imekumbwa na kasoro mbalimbali za mahesabu ikiwemo kukosekana kwa vibali vya kazi kwa baadhi ya raia wa kigeni wanaoshiriki kujenga mradi huo toka Dar es Salaam hadi Dodoma, jambo lililosababisha Serikali kukosa mapato. 

2. Tamasha la Urithi Wetu la kila mwaka lililopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii nalo limeibua utata mkubwa wa matumizi ya fedha, jambo lililozua mjadala mkubwa kwa sababu limehusisha vyombo vya habari, taasisi muhimu nchini. 

3. Huko Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) nako hakukubaki salama baada ya kusuasua kwa ukusanyaji wa mikopo ya wadaiwa.

Habari hii imeandikwa na Rodgers George, Gift Mijoe na Daniel Samson.