November 24, 2024

Robert Mugabe afariki dunia

Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mugabe kupitia ukurasa wake waTwitter

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa nchini Singapore ambako alikuwa anapatiwa matibabu kwa muda mrefu sasa. 

Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mugabe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95 kupitia ukurasa wake waTwitter. 

Amesema Mugabe alikuwa alama ya ukombozi, mtu wa Kiafrika aliyejitolea maisha yake kwa ukombozi na uwezeshaji wa watu wake. 

“Mchango wake katika historia ya Taifa letu na bara kamwe hautasahaulika. Nafsi yake ipumzike kwa amani ya milele!,” ameandika Rais Mnangagwa katika ukurasa wake wa Twitter,

Mugabe alikuwa moja wa viongozi wa Afrika waliokaa madarakani muda mrefu. Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipoondolewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Alizaliwa Februari 21, 924 nchini Zimbabwe. Atakumbukwa zaidi kwa uanamapinduzi wake ulioiwezesha #Zimbabwe kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. 

Ameacha mjane, Grace Mugabe, na watoto watatu; Bona Mugabe, Chatunga Bellarmine Mugabe, Robert Peter Mugabe Jr.