November 24, 2024

Sababu za kutazama filamu hizi mbili wiki hii

“Doctor Sleep” na “Midway”; filamu hizi zilizoingia sokoni hivi karibuni, zina visa vingi vya kufikirika lakini vyenye uhalisia wa maisha, zitaonyeshwa kwa wiki nzima kuanzia leo (Novemba 8, 2019) katika kumbi mbalimbali za sinema.

  • Moja inaelezea visa vya kutisha na kukung’atisha meno
  • Nyingine inakumbushia kisa cha vita ya pili ya dunia.
  • Yote ni kukujengea ujasiri wa kuyakabili yaliyopo mbele yako.

“Doctor Sleep” na “Midway”; filamu hizi zilizoingia sokoni hivi karibuni, zina visa vingi vya kufikirika lakini vyenye uhalisia wa maisha, zitaonyeshwa kwa wiki nzima kuanzia leo (Novemba 8, 2019) katika kumbi mbalimbali za sinema.

Moja ya ujumbe utakaopata ni ujasiri wa kuyakabili mambo yaliyopo mbele yako ili kufikia malengo uliyojiwekea. Lakini vitakuonyesha thamani ya mapumziko yako ya mwisho wa wiki. 

Doctor Sleep

Kama wewe ni msomaji wa vitabu na umewahi kukutana na kitabu cha “Doctor Sleep” basi hii ndiyo filamu yake. Chini ya kiogozi Mike Flanagan, filamu hiyo imegharimu kitita cha Sh103.7 bilioni akimuweka Danny Torrance (Ewan Mcgregor) kama “steringi” wa filamu hiyo.

Haitakufaa kama una moyo mwepesi kwani filamu hii ni kati ya zile zenye maudhui ya kutisha huku ikikuacha umeshikilia moyo wako mkononi.

Fuatilia filamu hii kuona namna nguvu za mazingaombwe na miujiza alizonazo Torrance aliyecheza filamu za “Jack the Giant Slayer”, “Star Wars” na “Son of a Gun” anazitumia kufariji watu wanaokaribia kukata roho.

Huku akiungana na magwiji wengine wakiwemo Rose (Rebecca Ferguson) aliyeigiza kwenye filamu lukuki zikiwemo za “Men in black”, “Greatest Showman” na “Mission Impossible-Fallout”.

Haitakufaa kama una moyo mwepesi kwani filamu hii ni kati ya zile zenye maudhui ya kutisha. Picha| Mtandao

Unahitaji kujua kama ataweza kushindana na “True Knot” ambao wao wanatafuta mvuke unaotolewa na mtu kabla ya kufa? Je ni kina nani? Siyo haba kujibu maswali hayo kwa Sh10,000 tu kutazama filamu hiyo katika kumbi zote za filamu Dar es Salaam.

Midway

Ni wakati mwingine wa kurudi vitani. Kuacha familia na kwenda kuchafua anga na mabomu na moshi mweusi ambao ni matokeo ya milipuko, kurusha mabomu kwenye meli kubwa za kivita na kucheza muziki kidogo na yule umpendaye.

Ikiwa chini ya kiongozi Roland Emmerich, “Midway” imegharimu Sh137.1 bilioni  ikisimulia kisa cha vita ya pili ya dunia iliyopiganwa kwa siku nne.

Fuatilia kisa hiki kuona namna gani majeshi ya anga ya Marekani yanapopigana na Mjapani yakiwahusisha waigizaji lukuki wakiwemo Luke Evans aliyeshiriki filamu kama “Dracula”, “Beauty and The Beast”, “The Hobbit Fast” an “Furious” na zingine zaidi ya 30.


Zinazohusiana


Haijaishia hapo. Yupo Bruno (Nick Jonas), Edwin Layton (Patrick Wilson) aliyeigiza zaidi ya filamu 40 ikiwemo ya “Aqua Man”. Pia Ane Best (Mandy Moore) ambaye ni sauti nyuma ya filamu ya “Tangled” na mwigizaji kwenye filamu ya “47 Metres Down”.

Kama zote hizi siyo mikato yako, bado Maleficent, Terminator na filamu zingine zinazobamba bado zinaonyeshwa kwenye kumbI hizo zikiwemo za Mlimani City na Aura Mall.