July 3, 2024

Sababu za wanyama kuhusika katika utengenezaji wa chanjo ya Corona

Ni kwa sababu wanaonyesha matokeo haraka ya majaribio ya utafiti wa chanjo.

Dar es Salaam. Zipo sababu mbalimbali zinazowafanya watafiti kutumia wanyama wakati wa utengenezaji wa chanjo mbalimbali ikiwemo ya COVID-19. Sababu mojawapo ni kuwa inawasaidia watafiti kufahamu kwa undani kuhusu ugonjwa husika na jinsi chanjo inavyoweza kufanya kazi ikianza kutumiwa na binadamu.