November 24, 2024

Shirika la ndege la Afrika Kusini lapigwa jeki kujifufua

Shirika hilo limepokea zaidi ya Sh600 bilioni ili kulisaidia kurejea kwenye biashara baada ya kufunga biashara Aprili, 2020.

  • Shirika hilo limepokea zaidi ya Sh600 bilioni ili kulisaidia kurejea kwenye biashara baada ya kufunga biashara Aprili, 2020.
  • Ili kubaki kwenye biashara, limefikia maazimio yakiwemo kupunguza nusu ya ndege na wafanyakazi wake.

Dar es Salaam. Shirikala Ndege la Afrika Kusini (SAA) linatarajia kupokea Sh609.29 bilioni kuliongezea nguvu tena ya kujiendesha baada ya misukosuko mbalimbali ikiwemo athari za Corona.

Hivi karibuni shirika hilo liliuza mali zake na kutangaza kuwafuta kazi wafanyakazi wake 4,700 ili kulifunga rasmi lakini mwezi Mei Serikali ya Afrika Kusini liliipa siku 25 kutangaza mpango wa kujifufua na kurudi katika soko ka ushindani.

Shirka hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa lilikuwa linahitaji takribani Sh266.1 bilioni za mtaji wa biashara, Sh266.1 bilioni nyingine kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi ambao waliachishwa kazi Aprili 30 na Sh80.96 bilioni kwa ajili ya kuwalipa wadeni wake.


Zinazohusiana


Hata hivyo, mpango mkakati uliotolewa na Shirika hilo ni pamoja na kupunguza idadi ya wafanyakazi kwa takribani asilimia 50 na kubaki na wafanyakazi 2,500, na kupunguza asilimia 50 ya ndege zake na kubaki na  ndege 20 tu.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Wallstreet, Mwezi Februari, Serikali ya Afrika Kusini ilitoa takribani Sh2.186 bilioni kwaajili ya kulipa madeni yote ambayo SAA inadaiwa huku madeni mengine ya muda mfupi yatalipwa Julai mwaka huu. 

Shirika la ndege la Afrika kusini limekuwa likipigania kubaki katika huduma ya anga tangu mwaka 2011 na kwa muda huo wote, limekuwa likitegemea msaada wa serikali kujiendesha na kubaki angani.

Je, muamko huo mpya unaweza kuleta mabadiliko? Endelea kusoma Nukta Habari (www.nukta.co.tz).