Shule 10 bora zilizotikisa matokeo kidato cha nne 2019
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato nne mwaka 2019 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri zikiongozwa na Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera ambayo imeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
- Necta imezitaja shule 10 zilizofanya vizuri zikiongozwa na Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera ambayo imeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
- Shule nyingine ni St. Francis Girls ya mkoani Mbeya, Feza Boys, Cannosa , Anwarite Girls, Precious Blood, na Marian Boys.
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato nne mwaka 2019 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri zikiongozwa na Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera ambayo imeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
Akitangaza matokeo hayo leo (Junuari 9,2020) Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amezitaja shule nyingine tisa zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo kuwa ni St. Francis Girls ya mkoani Mbeya ambayo mwaka juzi ilishika nafasi ya kwanza kabla ya kushushwa na Kemebos.
Nafasi ya tatu kwa mujibu wa Necta imeenda kwa Shule ya Sekondari Feza Boys ya jijini Dar es Salaam, Cannosa (Dar es Salaam), Anwarite Girls (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Marian Boys (Pwani).
Nyingine ni St. Augustine Tagaste (Dar es Salaam), Maua Seminary (Kilimanjaro) na Musabe Boys ya jijini Mwanza ambayo imeshika nafasi ya 10 kitaifa.
Soma zaidi:
Kwa matokeo hayo, hakuna hata shule moja ya Serikali iliyofanikiwa kuingia katika orodha hiyo dhahabu, kama ilivyokuwa mwaka juzi.
Katika orodha hiyo Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na shule tatu wakifuatiwa na Kilimanjaro ambayo imeingiza shule mbili huku mikoa ya Mbeya, Kagera, Mwanza, Arusha na Pwani zikiingiza shule moja moja.