July 8, 2024

Siri shule iliyoshika nafasi ya kwanza matokeo kidato cha nne

Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 wanafunzi wake 35 kati ya 70 wamepata daraja la kwanza alama saba.

  • Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 wanafunzi wake 35 kati ya 70 wamepata daraja la kwanza alama saba.
  • Meneja wa shule hiyo imesema siri ya ushindi ni nidhamu kwa walimu na wanafunzi.
  • Toka inaza kushiriki mtihani ya kidato cha nne  haijawi toka 10 bora.

Dar es Salaam. Katika matokeo kidato cha nne mwaka 2019 yaliyotangazwa Januari 9, 2019, Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera imeshika nafasi ya kwanza kitaifa, lakini ufaulu wake ulikuwa siyo kubahatisha.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), shule hiyo imeungana na shule zingine tisa ambazo zinaunda orodha ya shule 10 bora kitaifa. 

Kemebos siyo tu imeshika nafasi ya kwanza kitaifa lakini katika matokeo hayo pia imefanikiwa kufaulisha wanafunzi wake wote 70  katika daraja la kwanza ambapo wasichana walikuwa 26 na wavulana 44.

Asilimia 50 kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo katika shule hiyo wamepata daraja la kwanza la alama saba, ambapo  walikuwa 35 kati yao wasichana walikuwa 12.

Kemebos imevunja rekodi ya kuwa na wanafunzi 35 waliopata daraja la kwanza la alama saba tangu shule hiyo ilipoanzishwa. 

Licha ya kuweka alama hiyo shuleni hapo lakini hawajaweza kuvunja rekodi  ambayo imewekwa na shule ya Wasichana  ya Mtakatifu Francis ya Mkoani Mbeya ambapo katika matokeo hayo imevunja rekodi yake yenyewe kwa wanafunzi 57 kupata daraja la kwanza alama  saba  ukilinganisha na wanafunzi 41 waliopta alama hizo mwaka juzi.

Tunaweza kusema Kemebos imefanya maajabu kwa sababu mwaka 2017 na mwaka juzi ni mwanafunzi mmoja tu alipata daraja la kwanza alama saba. Lakini mwaka 2019 zimeongezeka hadi kufikia 35.


Zinazohusiana:


Matokeo ya Kemebos siyo ya kubahatisha 

Kama unadhani matokeo ya Kemebos ni ya kubahatisha utakuwa unakosea sana kwani katika kipindi cha miaka mitatu nyuma toka mwaka 2017 wamekuwa wakifanya vizuri.

Mwaka 2017, shule hiyo ilishika nafasi ya tatu kitaifa ambapo wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 42 ambapo 40 walipata daraja la kwanza na wawili daraja la pili.

Mwaka uliofuata ilikaza zaidi ikipanda hadi nafasi ya pili kitaifa kwa wanafunzi wake wote 58 waliofanya mtihani kupata daraja la kwanza kabla haijapanda kileleni mwaka jana na kuishusha St.Francis hadi nafasi ya pili. 

Meneja wa Shule ya Sekondari ya Kemebos, Eulogius Katiti amesema siri ya mafanikio yao ni mipangilio na mikakati walio jipangia shule hapo ya kuhakikisha walimu na wanafunzi wanashikiana kufanikisha ushindi wa shule hiyo. 

Amesema wamefanikiwa kuitafsiri nidhamu kwa kila mwanafunzi licha ya kuwa shule hiyo ni ya mchanganyiko ambapo watu wengi wanadhani mafanikio hayawezi kutokea.

‘’Tunafanya vizuri kwa miaka miwili mfululizo kwa sababu ya mipango tuliyojiwekea sambamba na nidhamu waliyo nayo wanafunzi’’amesema Katiti.

Hata hivyo, Kemebos itakuwa na kibarua kigumu cha kutetea nafasi yake ambayo imeshika katika matokeo hayo, ikizingatiwa shule mbalimbali zinafanya jitihada kuhakikisha zinaipata nafasi hiyo ya dhahabu