Taarifa muhimu kuhusu virusi vya Corona
Licha ya kuwa ugonjwa huo kuendelea kueneo katika maeneo mbalimbali duniani, Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ikiwemo kuosha mikono mara kwa mara
- Mpaka sasa virusi hivyo vimethibitishwa katika nchi 22 za Afrika.
- Rwanda na Kenya zimekuwa nchi za kwanza Afrika Mashariki kupata wagonjwa wa virusi hivyo.
Wakati hakuna mgonjwa yeyote aliyebainika kuwa ugonjwa wa virusi vya Corona Tanzania, nchi kadhaa ya Afrika zimeifunga mipaka na kuweka vizuizi katika safari za ndege kwa lengo la kuzuia kuenea kwa virusi vya corona ambavyo vimekwishathibitishwa katika nchi 26 za bara hilo.
Kati ya nchi hizo zipo mbili za Afrika Mashariki za Rwanda na Kenya.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza hali ya dharura kitaifa, na kuonya kuwa janga la virusi hivyo linaweza kuwa na athari za kudumu kwa uchumi wa nchi yake.
Naye Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia amepiga marufuku safari za ndege kutoka nchi zote ambako maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) yamekwisharipotiwa.
Shule na vyuo vikuu vimefungwa katika mataifa mengi ya Afrika sambamba na mikusanyiko yote ya hadhara, ikiwemo ya kidini.
Inaelezwa nchini Ghana, Rais Nana-Akufo Addo ameamuru shughuli za mazishi zisihudhuriwe na watu zaidi ya 25.
Licha ya kuwa ugonjwa huo kuendelea kueneo katika maeneo mbalimbali duniani, Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ikiwemo kuosha mikono mara kwa mara hasa baada ya kushika vitu katika maeneo yenye watu wengi.
Pia Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linawataka watu kutokugusa mdomo, macho au pua na kutakiwa kutumia tishu wakati wa kukohoa ua kupiga chafya. Baada ya matumizi tishu inatakiwa kutupwa sehemu salama.