July 8, 2024

Tafakari haya kabla ya kuingia kwenye ujasiriamali

Ni pamoja na kuwa na nia thabiti pia kuifahamu biashara unayotaka kuifanya.

  • Ni pamoja na kuwa na nia thabiti pia kuifahamu biashara unayotaka kuifanya. 
  • Hakikisha una wazo bora na mtaji wa kuendesha biashara.
  • Tafuta mshauri wa biashara ili kuepuka makosa.

Dar es Salaam. Wapo watu wengi wanatamani kujiajiri kwa kungia kwenye ujasiriamali lakini wanashindwa ni wapi waanzie.

Baadhi yao hufikiri  kuwa ufunguo wa kuingia kwenye ujasiriamali ni mtaji pekee, hawafahamu kuwa yapo mambo mengine wanayopaswa kuzingatia ili wafanikiwe katika kile wanachokifanya.

Miongoni mwa mambo hayo ni kuwa na msukumo binafsi katika biashara yako kwani wewe ndiyo una maono na biashara yako na siyo jirani, ndugu wala rafiiki zako.

Je, unahitaji nini ili uingie kwenye ujasiriamali, tazama video hii.