Tamasha kuwaunga mkono wapambanaji wa Corona kufanyika Aprili 18
Tamasha hilo ambalo hadi sasa limekusanya kitita cha Sh81 bilioni litahusisha wasanii wengine wakongwe wakiwemo Elton Johnn, Billie Eilish, Burna Boy, Johnn Legend na wengineo wengi wakiwemo Andrea Bocelli na Stevie Wonder.
- Litafanyika kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo Twitter, Instagramu na chaneli za televisheni.
- Hadi sasa limekusanya zaidi ya Sh80 bilioni kusaidia harakati za wadau wa afya kwenye kipindi cha mlipuko COVID-19.
- Lady Gaga ataungana na wasanii wengine kibao wakiwemo John Legend na Burna Boy.
Dar es Salaam. Licha ya kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona ambao umesababisha watu wasikusanyike pamoja, bado burudani ya muziki lazima iendelee.
Shirika la Afya Duniani (WHO) likishirikiana na Shirika la Utetezi wa Kimataifa la Global Citizen limeandaa tamasha la muziki la “Together At Home” yaani Pamoja Nyumbani linalolenga kuunga mkono juhudi za watumishi wa sekta ya afya wanaopambana na virusi vya corona.
“Tamasha hilo la mtandaoni litaonyesha umoja baina ya watu wote walioathirika na COVID-19 pamoja na kusherehekea na kuunga mkono mashujaa na watoa hudama za afya ulimwenguni wanaofanya kazi nzuri ya kuokoa maisha,” imesomeka taarifa ya Global Citizen.
Baadhi ya wadau watakaoonyesha tamasha la One worls: Together at home. Picha| The Verge.
Tamasha la “Together At Home “ ambalo mashirika hayo yameingia makubaliano na mwanamuziki wa miondoko ya muziki wa pop, Lady Gaga litaonyeshwa mubashara mtandaoni Aprili 18, 2020 kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo Youtube na mtandao wa Instagram.
Mifumo mingine itakayoonyesha tamasha hilo ni pamoja na televisheni za MTV, Tidal, NBC, Alibaba na chaneli za M-Net. Pamoja na hayo, mitandao ya Twitter na Yahoo pia haijaachwa nyuma.
Zinazohusiana
- Hawa ndiyo wanamuziki wa kike wanaotikisa dunia kwa wafuasi wengi Youtube
- Programu za mauzo zinazoweza kuwatoa wanamuziki wa Tanzania
- Wanafunzi vyuo vikuu waugeukia muziki kutoka kimaisha
Tamasha hilo ambalo hadi sasa limekusanya kitita cha Sh81 bilioni litahusisha wasanii wengine wakongwe wakiwemo Elton Johnn, Billie Eilish, Burna Boy, Johnn Legend na wengineo wengi wakiwemo Andrea Bocelli na Stevie Wonder.
Zaidi, watakaoendesha tamasha hilo ni pamoja na wachekeshaji Jimmy Fallon, Jimmy Kimmel na Stephen Colbert.
Lady Gaga amesema, “Tunawashukuru wafanyakazi wote wa sekta ya afya nchini na duniani kote ambao wamekuwa mstari wa mbele kwenye kipindi cha COVID-19… mnachokifanya kinawaweka nyie wenyewe kwenye hatari kuisaidia dunia na tunawaheshimu.”