July 5, 2024

Tanzania yatimiza mwaka mmoja tangu kuripoti mgonjwa wa kwanza wa Corona

Kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona nchini kilithibitishwa Machi 16, 2020 ambapo mgonjwa huyo alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 46.

  • Kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona nchini kilithibitishwa Machi 16, 2020 ambapo mgonjwa huyo alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 46.

Dar es Salaam. Leo Machi 16, 2021, umetimia mwaka mmoja tangu kutangazwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona nchini Tanzania. 

Kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona nchini kilithibitishwa Machi 16, 2020 ambapo mgonjwa huyo alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 46 ambaye aliwasili Tanzania  kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea Ubelgiji.

Mpaka sasa, Tanzania imeripoti visa vya Corona 509 huku kati ya wagonjwa hao, 21 wamefariki dunia.

Licha ya Serikali ya Tanzania kutokuweka hadharani takwimu za wagonjwa wa Corona tangu Mei 7 mwaka jana, imeendelea kuwasisitiza raia wake kuchukua hatua kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji, kutumia kitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.