November 24, 2024

Tozeni bili za maji zisizowaumiza wananchi-Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji ifuatilie utendaji wa mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na ihakikishe kwamba bili wanazotozwa wananchi zinakuwa na uhalisia na siyo kuwaumiza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12.2019. Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji ifuatilie utendaji wa mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na ihakikishe kwamba bili wanazotozwa wananchi zinakuwa na uhalisia na siyo kuwaumiza.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji ifuatilie utendaji wa mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na ihakikishe kwamba bili wanazotozwa wananchi zinakuwa na uhalisia na siyo kuwaumiza.

Ametoa agizo hilo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu upandaji wa bili za maji ambao hauna uhalisia kwa sababu Serikali ndiyo inayotoa fedha za miradi hiyo nchini.

”Serikali haitakubali wala haitoruhusu mwananchi anatozwa gharama kubwa za maji,” amesema Waziri Mkuu leo (Septemba 12, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbungewa Viti Maalumu, Mariam Kisangi, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu suala hilo.

“Yako maeneo ambayo mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji kumejitokeza wimbi la mabadiliko ya kupanda kwa bei za bili, mfano wilayani Maswa mkoani Simuyu bei imeongezeka kutoka sh. 5,000 hadi 28,000 kwa mwezi.

“Bei hizo hazina uhalisia na hakuna sababu ya mamlaka kutoza bei kubwa kiasi hicho na kuwafanya wananchi washindwe kumudu kulipia bili zao, wakati Serikali ndio imetoa fedha za kugharamamia uanzwishwaji wa miradi hiyo na haijadai kurudishiwa fedha hizo,” amesema Majaliwa. 

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ifuatilie bei za bili wanazotozwa wananchi ili kujiridhisha kama zinazingatia uwezo wa wananchi wengi kuzilipa hasa wale wa vijijini.