November 24, 2024

Tunayoyajua kuhusu shule 10 vinara kidato cha nne mwaka 2019

Jumla ya wanafunzi 870 walifanya mtihani kutoka kwenye shule hizo na kati ya wanafunzi hao 97 kati ya 100 walipata daraja la kwanza.

Dar es Salaam. Hivi karibuni Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, alitangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na nne ya mitihani iliyofanyika  Novemba 2019. 

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018 huku akizitaja shule10 bora kitaifa zikiongozwa na Kemebos na kufuatiwa na Shule ya St Francis Girls  ya Mbeya.

Licha ya kuzifahamu shule 10 vinara kidato cha nne mwaka 2019 zikiwemo nne za wasichana, kuna mengi ambayo hayakufahamika haraka kwa kuwa yalihitaji uchambuzi wa kina.

Haya ndiyo tunayojua kuhusu shule 10 bora kitaifa.