November 24, 2024

Twitter yazindua program mpya kupambana na habari za uzushi

Ni Birdwatch inayoruhusu watu kuripoti taarifa ambazo wanaamini ni za uongo kwenye mtandao.

  • Ni Birdwatch inayoruhusu watu kuripoti taarifa ambazo wanaamini ni za uongo kwenye mtandao.
  • Programu hiyo itawasaidia watumiaji wa mitandao ya kijamii kuzitambua na kung’amua habari za uzushi kuhusu Corona.

Dar es Salaam. Ili kuwa sehemu ya mapambano ya habari za uzushi duniani ikiwemo  zinazogusa janga la COVID-19, mtandao wa Twitter umeanzisha programu maalum ya  kukabiliana na habari hizo.

Programu hiyo ya Birdwatch itakuwa inafuatilia kwa karibu habari za uzushi kwenye mtandao huo na kisha kuzidhibiti zisiathiri watumiaji wake. 

Birdwatch itaanza kufanya kazi nchini Marekani kwa majaribo na baadaye itasambaa sehemu zingine ambapo kwa sasa yanakusanywa maoni ili kuiboresha ifanye kazi kwa ufanisi mzuri.

Mpango huo utaweza kufanya kazi nchi humo kwa mtumiaji yoyote wa Twitter isipokuwa watu wachache waliochaguliwa ndiyo watakaoweza kutoa maoni na kuchapisha kwenye “note”. 

Jinsi inavyofanya kazi

Kwa mujibu wa mtandao wa Twitter, Birdwatch inaruhusu watu kuripoti taarifa ambazo wanaamini ni za uongo kwenye mtandao huo wa kijamii kwa kutumia sehemu ambazo ni “notes” na rating.

Mtumiaji ataweza kutumia programu hiyo kwa kuandika ujumbe “write notes” na kwenda kwenye mtandao huo kulia juu ya kona ya Twitter ambapo ataona alama ya doti tatu (…).

Ataweza bonyeza hizo doti tatu chini kabisa ataona zana ya Birdwatch site itakayompa maelezo ya nini cha kufanya.

Twitter imeleza kuwa ili mtu aweze kutumia Birdwatch ni lazima afahamu thamani ya habari ambayo anairipoti ikwemo kukosoa kwa nia njema.


Zinazohusiana


Mtumiaji wa Twitter atatakiwa kwenda kwenye sehemu ya note ataona maoni ya watu wengine kuhusu hiyo habari iliyochapishwa kisha atatakiwa kuipima (rating) kutokana na maoni yaliyopo katika habari hiyo.

Zana hiyo mpya ya Twitter ni muhimu sana kwa wadau wanaopambana na habari za uzushi hasa zinazohusu COVID-19, janga ambalo linaitesa dunia kwa sasa.