November 24, 2024

Ubalozi wa China waanza kutumia mfumo wa kielektroniki kuomba visa

Utaratibu huo umeanza leo (Aprili 1,2019) ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa visa kwa watu wanaosafiri kwenda China.

  • Utaratibu huo umeanza leo (Aprili 1,2019) ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa visa kwa watu wanaosafiri kwenda China.
  • Kuanzia Mei 1, 2019 mfumo pekee wa kuomba visa utaokaokubaliwa ni kwa njia ya mtandao. 
  • Utaratibu huo hautawahusu wasafiri wanaelekea Hong Kong na Macao.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha inaongeza ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa visa, ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania leo umeanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa kuomba visa inayowawezesha watanzania kuingia China. 

Mfumo huo unajulikana kama ‘China online Visa application’ (COVA) ambapo ni hatua kubwa ya utumiaji wa mifumo ya kidijitali kurahisisha utoaji wa huduma ambapo sasa watu hawatalazimika kwenda katika ofisi za ubolozi huo kukamilisha maombi badala yake watafanya wakiwa popote nchini. 

Kwa mujibu wa taaarifa iliyotolewa na Ubalozi huo Machi 28, 2019 imeeleza kuwa utaratibu huo mpya unaanza kutumika leo Aprili 1, 2019 ambapo itawahusu waombaji wa visa ya Chinatu na wale wanaoomba visa ya  Hong Kong na Macao hawatahusika. 

Hata hivyo, kuanzia Aprili 1 hadi 30, 2019 mfumo wa zamani wa kuomba visa na mfumo mpya wa kutumia mtandao yote itakubaliwa.

“Hata hivyo, mfumo wa kuomba kwa njia ya mtandao utapewa kipaumbele na huduma kwa mfumo usio wa mtandao haitakuwa ya uhakika. Kuanzia Mei 1, 2019 mfumo pekee wa kuomba visa utaokaokubaliwa ni kwa njia ya mtandao,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo. 

Kwa mtu anayetaka kupata huduma za visa kwa njia ya mtandao atapata huduma hiyo kuanzia saa 2:30 hadi 5:30 asubuhi katika ofisi za ubalozi huo siku za kazi.

Sasa visa ya China unaweza kuipata kwa njia ya mtandao.|Picha Mtandao

 

Ili kukamilisha maombi kwa njia ya mtandao, mwombaji anatakiwa kukamilisha na  kutuma fomu ya kuombea visa ya mtandao kupitia tovuti ya https://voca.cs.mfa.gov.cn.

Pia kuchapa ukurasa wa uthibitisho na fomu ya COVA iliyokamilika kwa kutia saini ya uthibitisho, kuweka miadi kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kuomba visa kupitia tovuti iliyotajwa hapo juu na kisha mwombaji yeye mwenyewe kuwasilisha maombi yatakayojumuisha fomu ya COVA, ukurasa wa uthibitisho, uthibitisho wa AVAS, hati ya kusafiria na nyaraka nyingine kwenye ofisi ya visa ya Ubalozi wa China kwa mujibu wa muda wa miadi.


Soma zaidi:


Hatua iliyofikiwa na Ubalozi wa China ni muendelezo wa kurahisisha huduma za upatikanaji wa hati za kusafiria nchini ambapo Januari 1, 2018 Rais John Magufuli alizindua mfumo mpya wa kielektroniki wa utoaji hati ya kusafiria (E-passport). 

 Awali gharama za upatikanaji wa hati ya kawaida zilikuwa Sh50,000 lakini mfumo mpya umepandisha gharama mara tatu zaidi na sasa mtu anayefanya maombi ya pasipoti anatakiwa kulipa Sh150,000.

 Hata hivyo, Rais Magufuli alisema, “Kama mnavyofahamu nchi yetu ina passport yake, mfumo ulioitengeneza ni wa zamani hivyo kuruhusu wahalifu kuforge (kughushi). Passport tunayozindua leo ni ya kielektroniki na itakuwa ngumu kugushi, itasaidia kupeleka taarifa bila passport yenyewe.”