November 24, 2024

Uboreshaji mifumo ya uzalishaji vijijini kuwatoa vijana kimaisha

ili Tanzania na nchi nyingine za Afrika zikamilishe Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 inatakiwa kuzigeukia jamii za watu wanaoishi vijijini kwa kuboresha mifumo ya uzalishaji mazao ya kilimo.

Kutokana na uzalishaji mdogo katika sekta ya kilimo na viwanda, vijana wengi watapambana kutafuta ajira; matokeo yake na wale wanaokimbia kutoka vijijini kwenda mjini wataongeza na kuzidisha umasikini katika maeneo hayo. Picha|Mtandao.


  • Idadi ya vijana waishio Afrika walio na umri wa miaka kati ya 15 na 24 inatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya bilioni 90 ifikapo 2030, na idadi hiyo itakuwa maeneo ya vijijini.
  •  ili Tanzania na nchi nyingine za Afrika zikamilishe Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 inatakiwa kuzigeukia jamii za watu wanaoishi vijijini kwa kuboresha mifumo ya uzalishaji mazao ya kilimo.

Dar es Salaam.Ripoti ya Hali ya Chakula na Kilimo iliyotolewa na Shirika la Chakula Duniani mwaka 2017 imeeleza kuwa ili Tanzania na nchi nyingine za Afrika zikamilishe Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 inatakiwa kuzigeukia jamii za watu wanaoishi vijijini kwa kuboresha mifumo ya uzalishaji mazao ya kilimo.

Hiyo inatokana na ukweli kuwa  shughuli nyingi za kilimo zinafanywa na wananchi wanaoishi vijijini ambao wanapaswa kujengewa uwezo wa kiujuzi na teknolojia ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kukuza uchumi wa kaya.

Ikiwa Tanzania itafanikiwa kufanya mapinduzi ya kilimo vijijini ni dhahiri itachochea maendeleo ya viwanda na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.

Lakini wakati ikifikiri kufanya hivyo, kuna kila sababu ya kushughulikia changamoto ya kasi ya ongezeko la vijana na upatikanaji wa miundombinu endelevu ya kuwakwamua kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Ripoti hiyo ya FAO inaeleza kuwa kati ya mwaka 2015 na 2030, idadi jumuishi ya wakazi wa Afrika na Asia inatarajiwa kuongezeka kutoka 5.6 bilioni hadi zaidi ya 6.6 bilioni.

Inabainisha kuwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, idadi ya vijana walio na umri wa miaka kati ya 15 na 24 inatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya bilioni 90 ifikapo 2030, na idadi hiyo itakuwa maeneo ya vijijini.

Ongezeko hilo la vijana linaweza kutengeneza changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa karne zijazo. Kutokana na uzalishaji mdogo katika sekta ya kilimo na viwanda, vijana wengi watapambana kutafuta ajira; matokeo yake na wale wanaokimbia kutoka vijijini kwenda mjini wataongeza na kuzidisha umasikini katika maeneo hayo.


Soma zaidi:


Lakini tumaini bado lipo

FAO inashauri kuwa, ikiwa wananchi waishio vijijini wanataka kuondokana na umasikini ni muhimu kubaki katika maeneo yao kuliko kwenda mjini. Maamuzi hayo lazima yaende sambamba na mabadiliko ya sera zinazosimamia kilimo na kuongeza uwekezaji wa teknolojia utakaowawezesha vijana kulima kilimo cha kisasa.

Mshauri na Mtaalam wa masuala ya Biashara na Maendeleo kutoka taasisi ya Small Starter, John-Paul Iwouha amesema licha ya  maendeleo ya viwanda katika bara la Afrika kwenda taratibu, mabadiliko vijijini yanaweza kufanyika kwa kuinua mfumo wa uzalishaji chakula ili kufikia mahitaji ya wakazi waishio mjini

Amesema, “Lengo ni kuboresha mfumo wa chakula na kutengeneza fursa mpya za uchumi kwenye shughuli za kilimo ikiwemo kilimo cha biashara, uchakataji, usindikaji, usambazaji na utunzaji. 

Kuongezeka kwa mahitaji ya soko la vyakula kutoka mjini inatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko vijijini”.

Iwouha amesema ili kuhakikisha mabadiliko hayo yanamnufaisha kila mwananchi, watunga sera na Serikali wanapaswa kuelewa utendaji jumuishi wa jamii na uchumi wa miji, majiji na maeneo ya vijijini na jinsi unavyoweza kuimarisha mfumo wa uzalishaji chakula bila kuwaathiri wakulima wadogo.