October 6, 2024

Ufanye nini unapoona dalili za Corona kwa mwanafamilia?

Inashauriwa kumpatia chumba cha peke yake huku wanafamilia wengine wakichukua tahadhari.

  • Inashauriwa kumpatia chumba cha pekee yake huku wanafamilia wengine wakichukua tahadhari.

Dar es Salaam. Kutokana na baadhi ya shughuli za kijamii kuendelea, huenda baadhi ya wanafamilia wamekuwa wakichangama na mara kadhaa na watu wengine huku wakati mwingine wakisahau kuchukua tahadhari.

Kuchangamana huko kunaweza kutokea kazini, shuleni, maeneo ya  ibada na hata sehemu za starehe na endapo tahadhari stahiki haichukuliwi ipasavyo, kunakuwa na uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Endapo hali hiyo itatokea kwa mmoja ya mwanafamilia nyumbani kuna hatua muhimu za kuchukua ili kuhakikisha anahudumiwa vyema na kupunguza hatari ya kuwaambukiza wengine. Tazama video hii kufahamu nini cha kufanya ili kujikinga na maambukizi.