October 6, 2024

Ujerumani kuanza kutoa chanjo ya Corona kwa kila mtu Juni

Wakati Tanzania ikishauriwa kuanza kutoa chanjo ya Corona kwa raia wake, Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema nchi yake itaanza kutoa chanjo hiyo kwa kila mtu kuanzia Juni 7 mwaka huu.

  • Itaanza kutoa chanjo hiyo kwa kila mtu kuanzia Juni 7 mwaka huu.
  • Imesema inataka kuwakinga zaidi raia wake.
  • Tanzania yashauriwa kuanza kutoa chanjo kwa raia wake.

Wakati Tanzania ikishauriwa kuanza kutoa chanjo ya Corona kwa raia wake, Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema nchi yake itaanza kutoa chanjo hiyo kwa kila mtu kuanzia Juni 7 mwaka huu.

Mei 17, 2021, Kamati maalum ya iliyoundwa na Rais Samia Suluhu kuchunguza hali ya ugonjwa wa Corona nchini wakati ikiwasilisha ripoti yake ilipendekeza kuwa Serikali iruhusu matumizi ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwa Watanzania kwani ni salama na zimekidhi viwango vya kisayansi.

Waziri Spahn amewaambia waandishi wa habari jana Mei 18 kuwa mfumo wa sasa wa afya nchini Ujerumani hautazingatia kutoa kipaumbele kwa makundi maalum ya watu wakati wa utoaji chanjo kama ilivyokuwa awali.

Waziri huyo amesema kampeni ya chanjo imeshika kasi katika wiki za hivi karibuni na kwamba mwishoni mwa mwezi huu wa Mei, karibu asilimia 40 ya watu nchini Ujerumani watakuwa wamepata chanjo ya kwanza.


Soma zaidi: 


Amesema hadi sasa asilimia 70 ya wale walio juu ya umri wa miaka 60 tayari wamepokea chanjo ya kwanza na karibu robo yao wamekwisha pewa chanjo kamili. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, dozi za chanjo milioni 40 dhidi ya corona zimetolewa na karibu watu milioni 9  wamepewa chanjo kamili, katika nchi hiyo yenye watu milioni 83.

Mpaka sasa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Ujerumani imeripoti visa zaidi milioni 3.6 vya Corona na  vifo 86,671.