September 29, 2024

Uko tayari kupata chanjo ya Corona? Hili linakuhusu

Ili chanjo ifanye kazi kwa mtu aliyepata, ni lazima ukamilishe dozi zote zinazopendekezwa na wataalam wa afya.

Dar es Salaam. Chanjo ya Corona ni miongoni mwa silaha zinazotumika kwa sasa duniani kupambana na ugonjwa wa Corona. Ili chanjo ifanye kazi kwa mtu aliyepata, ni lazima ukamilishe dozi zote zinazopendekezwa na wataalam wa afya. 

Kinyume na hapo atakuwa katika hatari ya kupata maamubiki ya ugonjwa huo ambao bado unaitesa dunia.