November 24, 2024

Umeingia kwenye mahusiano mapya? Tanzama filamu hii

Ni filamu inayohusu mahusiano ya mwanadada Molly ambaye ameamua kuingia katika mahusiano mapya

  • Ni filamu inayohusu mahusiano ya mwanadada Molly ambaye ameamua kuingia katika mahusiano mapya.
  • Hata hivyo mpenzi huyo mpya anashindwa kuwa chagua la mzazi wake na hata rafiki zake.
  • Nafsi ya Molly inaingia sintofahamu baada ya kijana Gunnar kualikwa katika hafla bila ridhaa yake.

Dar es Salaam. Wewe na rafiki zako mna mpango gani katika msimu huu wa sikukuu? Kama hauna mpango wowote, huenda huu ukakusaidia.

Tazama filamu ya ”FriendsGiving” katia kumbi za sinema wikiendi hii. Iko hivi:

Baada ya kuachana na mpenzi wake Gunnar, Molly anaamua kuendelea na maisha yake. Anafunika kombe, ili mwanaharamu apite na kuamua kuanzisha mahusiano mapya na bwana mdogo anayejulikana kama Jeff.

Lakini Jeff anaonekana mdogo kwa Molly lakini nani alisema mapenzi yanaangalia umri? Hayupo.

Kama ilivyo sasa, kwa Molly naye ni mwisho wa mwaka na kuelekea siku ya kutoa shukrani, almaarufu kwa kimombo kama “thanksgiving” ambayo ni sikukuu ya kusheherekea mavuno ya mwaka mzima inayofanyika kila kati ya mwezi Oktoba na Disemba kila mwaka, anaamua kualika jopo la rafiki zake ili wajumuike nao.

Wakati wengine wanamshangaa kwanini ameingia kwenye mahusiano mapema kiasi hicho, mama yake anamualika Gunnar (mpenzi wake wa zamani) na hapo ndipo mashindano baina yake na Jeff yanapoanza.


Soma zaidi:


Wakati Gunnar anaonyesha uwezo wake wa kuwa mwanaume aliye na viwango na sifa zote, Jeff bado ana utoto kidogo unamsumbua na hivyo kushindwa kujijengea picha nzuri kwa rafiki wa Molly.

Kutazama filamu hii, jiandae kutarajia yasiyotarajiwa, kuona yasiyoonwa na kucheka zaidi ya ulivyowahi kucheka kwani wababe wa filamu za ucheshi akiwemo Deon Cole, Wanda Sykes na wengine kibao wanakungoja.

Kama filamu za ucheshi siyo fungu lako, filamu ya ‘Vanguard’ na katuni ya ‘The Crods 2’ pia zinaonyeshwa katika kumbi hizo.