October 6, 2024

Unavyoweza kuepuka magonjwa ya ngozi

Ni kwa kuepuka kuchangia nguo kwani yapo magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine.

  • Ni kwa kuepuka kuchangia nguo kwani yapo magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine.
  • Pia unatakiwa kunywa maji ili kuipatia afya nzuri ngozi yako.

Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi huja kwa namna nyingi na hutofautiana kati ya mtu na mtu. Wapo ambao hupata muwasho, wapo ambao ngozi hubanduka na wapo wapatao mba.

Magonjwa hayo husababishwa na mengi lakini mara nyingi huwa ni mtindo maisha, lishe, mzio na kuambukizwa na wengine.

Mfano, kwa mtindo maisha, wapo watu ambao hushindwa kujikausha vyema wanapomaliza kuoga hasa sehemu za miguuni na sehemu za siri na hivyo kuishia kupata fangasi katika maeneo hayo.

Ili kuepukana na tatizo hilo katika ngozi yako, unaweza kuangazia baadhi ya suluhu hizi: