October 6, 2024

Unavyoweza kujikinga na magonjwa ya figo

Ni kupitia kufanya mazoezi, kula mlo kamili na kunywa maji ya kutosha.

  • Magonjwa ya figo humpata mtu kutokana na mtindo maisha wake ikiwemo mazoea ya kufanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha.

Dar es Salaam. Mtindo wa maisha huwa na athari nyingi kiafya bila baadhi ya watu kufahamu. Mfano kushindwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi pamoja na kuwa mwangalifu kwa chakula unachotumia inaweza kuwa sababu ya kupata magonjwa mbalimbali yakiwemo ya figo.

Kwa mujibu wa tovuti ya elimu juu ya afya ya figo, ulaji wa chakula kilicho na chumvi nyingi, mlo usio kamili na kutokunywa maji ya kutosha huweza kumsababishia mtu kupata magonjwa ya figo.

Zaidi, katika video hii.