October 7, 2024

Unavyoweza kumsaidia mtoto kutimiza ndoto za maisha

Mambo hayo ni pamoja na kumfundisha michezo na stadi za kazii, kunoa kipaji chake na kumsikiliza kujua anataka nini.

  • Ni pamoja na kukuza kipaji chake na kujitahidi kugundua kitu anachokipenda.
  • Msikilize na mpe nafasi ya kutoa mawazo kuhusu mstakabali wake. 

Dar es Salaam. Kuna mambo mengi ambayo unaweza kumsaidia mtoto wako akiwa kwenye hatua za awali za ukuaji ambayo yatamsaidia kutimiza ndoto zake za maisha atakapokuwa mtu mzima.

Mambo hayo ni pamoja na kumfundisha michezo na stadi za kazii, kunoa kipaji chake na kumsikiliza kujua anataka nini. 

Mkazi waJijini Dar es Salaam Alma Miraj ambaye ni mama wa watoto wawili anasema kumweka mtoto wako karibu na vitu anachopenda akiwa mdogo, inamjengea mazoea na upendo na kitu hicho na hivyo kadri muda unavyozidi kwenda anakua bora kwenye jambo hilo.

“Mwanangu mwenye miaka sita anapenda sana kompyuta kwa hiyo baba mtu ameshamnunulia kompyuta na hivi karibuni ataanza kujifunza lugha za kompyuta (coding) maalumi kwa ajili ya watoto. 

“Mdogo wake anapenda shughuli za bustani kwa hiyo mara nyingi huwa na harakati nje ya nyumba. Bado tunawajenga kwenye vitu vingine kugundua kipi wanapenda zaidi,” amesema Alma.