October 6, 2024

Unavyoweza kuthibitisha habari za chanjo ya Corona Instagram

Ni pamoja na kuhakikisha unasoma zaidi kuhusiana na habari hiyo kupitia vyanzo rasmi ikiwemo WHO.

  • Unashauriwa kuthibitisha uthabiti wa ukurasa ambao umepata taarifa zinazohusiana na chanjo ya Corona.
  • Mara nyingi, kurasa za mashirika makubwa ya habari zimethibitishwa kwa kuwa na tiki ya bluu.

Dar es Salaam. Kupata habari sahihi kuhusu chanjo ya Corona huenda ikawa ni ngumu kwa sasa kama haufahamu sehemu maalumu ya kupata habari hizo.

Wengine wanatumia njia za habari rasmi ikiwemo habari zinazotolewa na vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo televisheni, magazeti na redio.

Hata hivyo, kundi ambalo lipo kwenye hatari ya kupata habari ambazo zinaweza kuwa ni za kupotosha ni wanaotumia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram kupata habari hizo.

Unawezaje kuthibitisha habari kuhusu Corona katika mtandao wa Instagram? Tazama video hii kujifunza zaidi.