Undani wa habari zinazopotosha kuhusu COVI-19
Zinakuja kwa mtindo mbalimbali ikiwemo upotoshaji wa maudhui (Misleading content).
- Zinakuja kwa mtindo mbalimbali ikiwemo upotoshaji wa maudhui (Misleading content).
- Misleading Content ni pale mtu anapochukua sehemu ya nukuu ambayo anaikusidia yeye na kuacha sehemu nyingine ya nukuu kwa nia ya kupotosha.
- Kabla ya kusambaza habari picha au takwimu ujiulize habari hiyo ina ukweli kiasi gani.
Dar es Salaam. Ukuaji wa teknolojia umefanya habari nyingi kupatikana kwa urahisi na kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja lakini kwa upande mwingine umesababisha kuongezaka kwa wimbi la taarifa za uzushi na uongo hasa wakati wa majanga kama ugonjwa wa COVID-19.
Miongoni mwa habari hizo za uzushi ni zile zinakuja na maudhui yanayopotosha (misleading content) ambazo mara nyingi zimekuwa zikileta taharuki na madhara kwenye jamii.
Aina hii ya habari ya upotoshaji imekuwa zikitumika kwa nia ovu na mara nyingine bila kujua kuwa habari husika ni ya kupotosha.
Mfano wa “misleading content” ni pale mtu anapochukua sehemu ya nukuu iliyopo kwenye habari ambayo anaikusidia yeye na kuacha sehemu nyingine ya nukuu kwa nia ya kupotosha au kutumia sehemu ya takwimu kwa ajili ya manufaa yake bila kuleza hizo takwimu zimepatikanaje.
Wakati mwingine kuchukua hata picha na kuchukua kipande cha picha na kukionyesha katika habari yake sambamba na kukiongezea maneno mengine kwa nia ovu ya kumuumiza muhusika mwingine.
Zinazohusiana:
Aina hii ya upotoshaji imekua ikitumika zaidi kuzua taharuki hasa za virusi VYA covid-19 ili kuwaumiza watu kwenye jamii. Kwa mfano mwisho mwa mwaka 2020, watu wenye nia ovu walitumia picha ya Meya wa London wa Uingereza, Sadiq Khan aliyopigwa wakati anapata chanjo ya mafua na kuitumia kuwa alikua anapata chanjo dhidi ya Corona.
Ili kuibaini aina hiyo ya habari ya upotoshaji unahitaji kutumia zana za kidijitali ikiwemo ‘Google Image Explore’ ambazo zinasaidia kukufahamisha uhalali wa habari au picha na ilikochukuliwa.
Pia ukipata habari ambayo unafikiri una mashaka nayo, usiisambaze kwa haraka, jipe muda wa kutafuta ukweli wake ili kupunguza madhara ya habari za uzushi kwenye jamii hasa wakati huu dunia ikipambana na janga la Corona.