July 5, 2024

Usidanganyike inzi hawaenezi ugonjwa wa Corona

WHO imesema hakuna taarifa wala ushaidi wa kuthibitisha kuwa inzi wanaeneza COVID-19.

  • WHO imesema hakuna taarifa wala ushaidi wa kuthibitisha kuwa inzi wanaeneza COVID-19.
  • Virusi vya COVID-19 vinasambaa kupitia maji maji wakati mgonjwa anapiga chafya, kukohoa au kuzungumza. 

Dar es Salaam. Habari za uzushi bado zinaendelea kushika kasi hasa katika mitandao ya kijamii ambako kuna watumiaji wengi wa taarifa za mtandaoni. 

Safari hii mdudu inzi ambaye ni maarufu katika nyumba za kuishi, naye anahusishwa na kueneza ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) kwa sababu hutua katika maeneo ambayo yanashikwa na watu wengi. 

Hata hivyo, dhana hiyo haina ukweli wowote. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa wala ushaidi wa kuthibitisha kuwa inzi wanaeneza COVID-19.

“Virusi vinasababisha COVID-19 kimsingi vinasambaa kupitia maji maji wakati mgonjwa anapiga chafya, kukohoa au kuzungumza,” imesema WHO katika taarifa yake ya kukanusha uvumi huo.


Zinazohusiana


Unaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa kushika maeneo yenye virusi kisha kugusa macho, pua na mdomo kabla ya kuosha mikono yako na siyo inzi akikugusa au kutua katika eneo ambalo umegusa. 

Kujikinga na ugonjwa huo, WHO bado inasisitiza kuwa kaa umbali wa mita moja na mtu mwingine, osha mikono yako kwa sababu na maji tiririka na epuka kugusa macho, pua na mdomo.

Pia vaa barakoa na epuka mikusanyiko isiyo ya lazima. 

Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ya Twitter/Facebook: @NuktaFakti na Instagram: @nuktafakti