November 24, 2024

Viza za matembezi zinavyochangamkiwa Tanzania

Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zinaeleza kuwa viza kwa ajili ya matembezi zilizotolewa kati ya Julai 2019 na Machi 2020 zilikuwa asilimia 93.8 ya viza zote 335,043 zilizotolewa kipindi hicho.

  • Viza kwa ajili ya matembezi zilizotolewa kati ya Julai 2019 na Machi 2020 zilikuwa asilimia 93.8 ya viza zote 335,043 zilizotolewa kipindi hicho.
  • Viza hizo hutolewa kwa wageni wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali. 

Dar es Salaam. Kama ulikuwa hujui wageni wengi kutoka nje ya nchi wanaoomba viza ya kuingia Tanzania wanakuja kwa shughuli za matembezi. 

Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zinaeleza kuwa viza kwa ajili ya matembezi zilizotolewa kati ya Julai 2019 na Machi 2020 zilikuwa asilimia 93.8 ya viza zote 335,043 zilizotolewa kipindi hicho. 

Wagani hao wanaokuja kwa ajili ya matembezi, wengine hutembela maeneo ya vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kupata muda wa kupumzika. 


Zinazohusiana


Hata hivyo, kwa kipindi hicho Tanzania imeongeza raia 87 wa kigeni kutoka nchi 13 waliotimiza vigezo vya kisheria ambao wamepewa Uraia wa Tanzania. 

Raia hao wametoka katika nchi za Kenya, Afganistan, Afrika Kusini, Rwanda, Lebanon na Somalia.

Wengine ni kutoka Italia, Pakistan, Uganda, Uingereza na Yemeni huku kati ya hao 87 mmoja alikuwa hana uraia wa nchi yoyote.