Wachimbaji wadogo wa madini Geita kupata mkopo kuendeleza rasilimali zao
Wameshauriwa kujiunga katika vikundi kwa sababu Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.
Wachimbaji wadogo wakichenjua madini kwa kutumia njia za kienyeji ili kujipatia kipato. Picha| Muungwana.
- Wameshauriwa kujiunga katika vikundi kwa sababu Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.
- Wameshauriwa kujiunga katika vikundi kwa sababu Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.
- Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo wanawezeshwa kufanya shughuli zao vizuri, Serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya kuwagawia wachimbaji hao.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewashauri wachimbaji wadogo wadogo mkoani Geita wajiunge katika vikundi ili Serikali iwapatie misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji ya kuendeleza rasimali za madini zinazowazunguka katika maeneo yao.
Amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.
Majaliwa ameyasema hayo leo (Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, wachimbaji hao wameshauriwa kujiunga katika vikundi kwa sababu Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.hasa dhahabu kwa lengo la kujiongozea tija.
Majaliwa ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.
Zinazohusiana: Maadhimisho ya Tanzanite yaahirishwa kupisha maombelezo ajali ya Mv Nyerere.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema wilaya ya Mbogwe inafanya vizuri katika sekta ya madini, ambapo ina viwanda 27 vya kuchenjulia dhahabu.
Katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo wanawezeshwa kufanya shughuli zao vizuri, Serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya kuwagawia wachimbaji hao.
Akizungumzia kuhusu leseni za uchimbaji mkoani Geita amesema kuna jumla ya leseni 971 za uchimbaji mdogo wa madini na kati yake zinazofanya kazi ni leseni 184 tu.
Biteko amewataka wachimbaji wadogo wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji kwenye maeneo yao waliyopangiwa na kwamba hakuna atakayewaondoa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
“Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Mbogwe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao,” amesema Majaliwa.
Awali, Majaliwa alikagua na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbogwe katika kijiji cha Kasosobe. Ujenzi huo utagharimu Sh4.3 bilioni. Pia alikagua mradi wa uboreshaji miundombinu na kuzindua maabara ya Kituo cha Afya Masumbwe.