October 6, 2024

Wagonjwa wa Corona wazidi kuongezeka Tanzania

Wagonjwa wengine 14 watangazwa leo na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufikia 46.

  • Wagonjwa wengine 14 watangazwa leo na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufikia 46.
  • Kati yao waliogundulika leo, 13 wapo Dar es Salaam na mmoja yupo jijini Arusha.

Dar es Salaam. Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) nchini Tanzania imeendelea kuongezeka baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kutangaza ongezeko la wagonjwa wapya 14 na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufika 46 hadi sasa.

Wagonjwa hao wapya, ambao ni wengi kuwahi kuripotiwa kwa siku moja tangu mgonjwa wa kwanza agundulike Machi 16,  wameongeza idadi ya waliokutwa na madhira ya COVID-19 kutoka watu 32 walioripotiwa awali Aprili 10, 2020.

Waziri Ummy katika taarifa yake iliyotolewa leo (Aprili 13, 2020) amesema wagonjwa wote 14 ni Watanzania ambapo 13 wanatoka katika Mkoa wa Dar es Salaam na mmoja yupo katika Mkoa wa Arusha.


Soma zaidi:Tafakari haya msimu wa sikukuu ya Pasaka


Idadi hiyo mpya ya wagonjwa wa COVID-19 inafanya Dar es Salaam kuendelea kuwa kitovu cha ugonjwa huo ambao umeshaua watu watatu hadi sasa.

Hadi leo Dar es Salaam imeripotiwa kuwa na wagonjwa 32 kati ya 46 waliotangazwa nchini. Hii ni sawa na kusema kuwa wagonjwa saba kwa kila 10 walioripotiwa Tanzania wapo Dar es Salaam.

“Wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam wa afya. Ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa unaendelea,” amesema Ummy katika taarifa hiyo.

Aidha, amewataka Watanzania kuendelea kuzingatia miongozo ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kutokugusa pua, mdomo au macho, kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

Pia kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na ikiwezekana kutulia nyumbani.  

Wagonjwa wa Corona wazidi kuongezeka Tanzania

aarifa iliyotolewa na Waziri huyo leo (Machi19, 2020), hadi sasa Tanzania ina wagonjwa sita ambapo watano wanatokea Tanzania bara na mmoja anatokea Zanzibar kama ilivyoripotiwa jana Machi 17, 2020.

  • Wizara ya Afya yathibitisha wagonjwa wengine wawili wa Corona leo na kufanya jumla ya wagonjwa kuwa sita mpaka sasa.
  • Wagonjwa wote wawili ni Watanzania walioingia nchini kwa nyakati tofauti. 
  • Serikali yawataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amethibitisha kuongezeka kwa visa vingine viwili vya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania na kufanya jumla ya wagonjwa kufikia sita. 

Taarifa iliyotolewa na Waziri huyo leo (Machi19, 2020), hadi sasa Tanzania ina wagonjwa sita ambapo watano wanatokea Tanzania bara na mmoja anatokea Zanzibar kama ilivyoripotiwa jana Machi 17, 2020. 

“Wagonjwa wapya wawili wamethibitika jijini Dar es salaam kuwa na Covid-19, na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa waliothibitika nchini mpaka sasa kufikia 06 (sita), ambapo mmoja ni yule wa Zanzibar aliyetolewa taarifa jana,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo, Ummy amesema wagonjwa wote wawili ni Watanzania, wanaume wenye umri wa miaka 40 kila mmoja.

Mmoja alisafiri nchi za uswisi, Denmark na Ufaransa kati ya Machi 5, 2020 hadi Machi 13 na kurejea nchini Machi 14.

Mwingine alisafiri kwenda Afrika Kusini kati ya Machi14, 2020 hadi Machi 16 na kurudi nchini usiku wa Machi 17.

Wagonjwa hao wametengwa na juhudi za kuendelea kuwafuatilia watu waliokuwa nao karibu zinaendelea.

“Wahusika wote wametengwa (isolation) na hali zao zinaendelea vizuri. Juhudi za kufuatilia watu waliokuwa karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na COVID-19 (yaani “contacts”) zinaendelea,” amesema Ummy.

Aidha, amebainisha kuwa hadi sasa jumla ya watu 46 wanafuatiliwa jijini Arusha, na watu 66 wanafuatiliwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania ilithibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo  Machi 16, na visa vitatu viliongezeka jana huku kimoja kikiripotiwa Zanzibar.


Zinazohusiana


Mpaka sasa ni nchi tatu za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya na Rwanda ndiyo zimethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi vya Corona, ambapo  jana Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema barani Afrika kuna kesi 233 za watu walioambukizwa. 

Wananchi wameshauriwa kuwa watulivu na kuchukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka za afya nchini ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kugusa mdomo, pua na macho. 

Pia kutumia tishu wakati wa kukohoa na kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima.