Wakulima wahimizwa kuongeza uzalishaji wa mazao msimu wa mvua za vuli
Mvua hizo za vuli ambazo huanza Oktoba hadi Desemba ni mahususi kwa maeneo ya nchi yanayopata vipindi viwili vya mvua kwa mwaka ambapo hujumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, Ukanda wa Pwani ya Kaskazini na Nyanda za juu Kaskazini Mashariki.
- Mvua hizo za vuli ambazo huanza Oktoba hadi Desemba ni mahususi kwa maeneo ya nchi yanayopata vipindi viwili vya mvua kwa mwaka ambapo hujumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, Ukanda wa Pwani ya Kaskazini na Nyanda za juu Kaskazini Mashariki.
- Wakulima wakumbushwa kupanda mazao yanayokomaa muda mfupi.
Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewataka wakulima katika mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka, kutumia vizuri mvua za vuli zinazoendelea kunyesha kuzalisha mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ili kujipatia kipato kutokana na kilimo hicho.
Taarifa iliyotolewa leo (Novemba 27, 2019) na Wizara ya Kilimo, inaeleza kuwa mvua hizo tayari zimeanza kunyesha katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Morogoro na zikitumiwa vizuri zitaleta manufaa makubwa.
“Wakulima wanahamasishwa kutumia vizuri mvua hizi kwa kupanda kwa wakati,” anasema Hasunga katika taarifa hiyo.
Aidha, Waziri Hasunga amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuwasimamia Maafisa Ugani Kilimo ili waweze kuwasaidia wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kupanda mbegu bora kulingana na kanda za kiekolojia na kutumia mbolea inayostahili kwenye mazingira husika.
Wizara ya Kilimo imesema itaendelea kutoa ushauri wa kitaalam na maelekezo kwa wakulima na wananchi nchini kuhusu mwenendo wa mvua na hatua za kuchukua ili kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ya kutosha na hatimaye nchi kuwa na usalama wa chakula.
- TMA yatahadharisha ujio mvua kubwa
- Watanzania washauriwa kutumia taarifa za hali ya hewa kwenye mipango ya maendeleo
- Ujio mfumo wa taifa wa hali ya hewa kuchochea ujenzi wa viwanda nchini.
Mvua hizo za vuli ambazo huanza Oktoba hadi Desemba ni mahususi kwa maeneo ya nchi yanayopata vipindi viwili vya mvua kwa mwaka ambapo hujumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, Ukanda wa Pwani ya Kaskazini na Nyanda za juu Kaskazini Mashariki.
Septemba 3, 2019, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitoa mwelekeo wa msimu za vuli za Oktoba hadi Desemba ambapo ilisema mvua katika kanda hizo tatu utatofautiana na hivyo tahadhari na mambo ya kufanya yanaweza kutofautiana.
Kuwepo kwa tofauti ya mvua kunasababishwa na mifumo ya hali hewa hasa joto la bahari na mvumo wa upepo kuelekea nchi kavu.
Hata hivyo, TMA ilieleza kuwa wananchi wanapaswa kujiandaa na kutumia vizuri mvua hizo kwa sababu zitakuwa za kutosha.