October 6, 2024

Wanachoweza kufanya wazazi kuwakinga watoto dhidi ya Corona

Ni pamoja na kuongea na watoto na kuwanunulia mahitaji muhimu ya kujikinga na Corona

Dar es Salaam. Usalama wa watoto huenda ikawa ni changamoto kubwa kwa walimu, wazazi na hata wanajamii kwani huenda wengi wanaumiza vichwa kwa kujiuliza ni kwa namna gani watoto wanaoenda shule wanaweza kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Hata hivyo, yote yanaweza kuanza nyumbani ambapo mzazi au mlezi anaweza kumfundisha mtoto wake jinsi ya kuchukua tahadhari.

Tazama video hii kufahamu namna mzazi au mlezi anaweza kumfundisha mtoto wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.