July 8, 2024

Waziri Mkuu atoa Siku 21 kwa Viwanda vya Vileo

TRA isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.

  • TRA isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.
  • Wizara na Taassi za Umma ziwe zimejiunga na Mfumo wa Serikali wa Kieletroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (GePG) Kabla ya Juni.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 21 kwa viwanda vyote vinavyozalisha vileo nchini viwe vimefunga mfumo ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za kielektroniki.Pia ameziagiza Wizara na Taasisi zote za Umma ziwe zimejiunga na Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli (GePG) kabla ya Juni mwaka huu.

Ametoa maagizo hayo jana (Jumamosi, Februari 9, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja, Bungeni jijini Dodoma.

Majaliwa  amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari 28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.

“Naielekeza TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutumia stempu za kielektroniki kwa viwanda vyote vinavyozalisha vinywaji hivyo.”amesema Majaliwa.

Pia,amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha na rasilimali za umma ili kufikia malengo.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kutumia mfumo wa kielektroniki wa stempu za kodi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa na zile zinazoingizwa nchini. 

Waziri Mkuu amesema mfumo huo utasaidia Serikali katika kupata taarifa sahihi za uzalishaji na kupunguza uvujaji wa mapato ya Serikali.

.