July 3, 2024

Zaidi ya nusu ya wagonjwa wa Corona wapona Afrika

Hadi jana Desemba 4, 2020 bara hilo limeripoti visa milioni 2.3.

Dar es Salaam. Wakati wagonjwa wa Corona wakiendelea kuongezeka Afrika, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinazonyesha kuwa zaidi ya nusu ya wagonjwa wanaopata COVID-19 wamepona barani humo. 

Takwimu za WHO za Desemba 4, 2020, zinaonyesha watu waliopona COVID-19 barani humo ni milioni 1.8 kati ya wagonjwa milioni 2.3 walioripotiwa kupata maambukizi. 

Hata hivyo, nchi ya Afrika Kusini imeendelea kurekodi kiwango cha juu cha wagonjwa wa COVID-19 barani humo.