November 24, 2024

Zifahamu sababu zinazowafanya vijana kujiua duniani

Kwa baadhi, changamoto za maisha zinawafanya wakose tumaini na hivyo kukatisha maisha yao.

  • Ni pamoja na watu kushindwa kuona suluhu ya matatizo wanayopitia.
  • Wengine hujiua kwa sababu ya unyanyapaa wa shuleni au nyumbani.
  • WHO imeshauri kufanya programu za vijana zinazowawezesha kukabiliana na msongo wa mawazo.

Dar es Salaam. Huwa unapata hisia gani unaposikia mtu fulani amejiua? Kwa wengine kujiua ni njia ya kukatisha matatizo ambayo yanawakabili huku wengine wakichukulia kitendo hicho kama mkosi unaoachwa katika familia au jamii kwa ujumla.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema matukio ya kujiua yanaripotiwa zaidi katika nchi ambazo zina uchumi wa chini pamoja na wa kati. 

WHO imesema inakadiriwa kuwa, kwa mwaka watu 800,000 hujiua huku njia hiyo ikiwa ni chanzo cha vifo vingi vya watu wenye umri wa miaka 15-29. 

“Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya matukio ya kujiua duniani yanatokana na watu kunywa sumu za wadudu, na matukio mengi hutokea katika vijiji vinavyojishughulisha na kilimo,” inasomeka sehemu ya makala ya WHO ya Septemba 2019 na kubainisha kuwa asilimia 79 ya vifo vya kujiua vinatokea katika nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati.

Je, kwanini watu huchagua kujiua? Tazama video hii ili ujifunze na kupata sababu za kutafuta msaada pale unapopitia hali kama zinazotajwa.