WhatsApp kuendelea na sera yake mpya ya faragha yenye utata
Ni sera ya faragha ambayo imeibua mjadala mpana duni kuhusu usiri wa taarifa za watumiaji wake.
- Ni sera ya faragha ambayo imeibua mjadala mpana duni kuhusu usiri wa taarifa za watumiaji wake.
- Yasema itaanza kuwakumbusha watumiaji wake kuipitia na kukubali masasisho ya sera hiyo ili kuendelea kupata huduma za jukwaa hilo la mtandaoni.
Mtandao wa WhatsApp ambao unamilikiwa na kampuni ya Facebook Inc umesema utaendelea na mchakato kusasisha (update) sera yake mpya ya faragha yenye utata iliyoibua mjadala mpana duniani.
Wakati ikiendelea kusasisha sera hiyo, itawawezesha watumiaji wake kuisoma kwa muda wao huku ikitoa tangazo la taarifa za ziada kuhusu sera hiyo.
Mapema January mwaka huu, jukwaa hilo la mawasiliano ya ujumbe mfupi liliwatangazia watumiaji wake kuwa linaandaa sera mpya ya faragha ambayo kwa sehemu itashirikisha taarifa zao binafsi na mtandao wa Facebook na makundi mengine inayoyasimamia.
Tangazo hilo liliibua mjadala mpana duniani huku baadhi ya watumiaji wakichukua maamuzi magumu ya kuhamia Telegram na Signal ili kulinda taarifa zao.
- Uunganishwaji wa WhatsApp, Facebok bado sana
- WhatsApp inavyowabeba wajasiriamali Tanzania
- Wadau mtandaoni watoa neno WhatsApp kudhibiti habari za uongo
Kutokana na suala hilo, WhatsApp ilisogeza mbele uzinduzi wa sera hiyo hadi Mei mwaka huu badala ya tarehe ya awali ya mwezi Februari ili kutoa fursa ya kuwaelimisha watumiaji wake juu ya mabadiliko hayo mapya.
Hata hivyo, Februari 18 mwaka huu katika blogu yake, WhatsApp imesema itaanza kuwakumbusha watumiaji wake kuipitia na kukubali masasisho ya sera hiyo ili kuendelea kupata huduma za jukwaa hilo la mtandaoni.
“Pia tumejumuisha taarifa zaidi kujaribu na kutatua malalamiko ambayo tunayasikiliza, imeeleza sehemu ya blogu hiyo.
WhatsApp itafanikiwa?